Home KITAIFA EWURA YAZITAKA MAMLAKA ZA MAJI NCHINI KUTOWAKATIA WATEJA WAO SIKU ZA...

EWURA YAZITAKA MAMLAKA ZA MAJI NCHINI KUTOWAKATIA WATEJA WAO SIKU ZA MWISHO MWA JUMA

Na Esther Mnyika, Dar es Salaam 

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nisahati na Maji (EWURA) imezitaka mamlaka za maji nchini kuacha kukata huduma ya maji kwa wananchi siku ambazo sio za kazi na badala yake watumie siku za kazi kusitisha huduma za maji kwani kufanya hivyo wanakiuka mkataba wa huduma kwa wateja kwa kukata maji siku zisizo za kazi.

Hayo yamebainishwa Disemba, 13 2024 jijini Dar es Salaam na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, wakati wa Mafunzo  ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji  kwa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA).

Amesema lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo wanahabari kutoa taarifa za sekta ya nishati na maji kwa usahihi na kwa wakati kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

“kumekuwa na ukiukwaji wa sheria za huduma kwa wateja baina ya mamlaka na wateja , kama Kukata maji siku zisizo za kazi na kusoma bili za maji bila kuhusisha wateja, wanakiuka mkataba wa huduma kwa wateja,”amesema.

Amefafanua kuwa EWURA ilitolewa miongozo huko nyuma ambayo inataka wasomaji wa mita za maji uwe unafanyika  wakati mmiliki wa mita yupo  eneo  hilo.

Kaguo amesema wana wahamasisha watanzania kusoma mikataba ya huduma kwa wateja kwa mamlaka mbalimbali  walizonazi.

Kwa upande wake  Kaimu Meneja wa EWURA, Kanda ya Mashariki, Mhandisi Mwanamkuu Kanizio amewakumbusha mafundi wanaofanya utandazaji nyaya kwenye majengo mballimbali kuhakikisha wanapata leseni za utandazaji waya kwani, kufanya kazi hiyo bila leseni ni kosa kesheria.

Amesema  EWURA inawajibu wa kutoa leseni  kwa mafundi umeme  ambao wanafanyakazi za utandazaji  waya kwenye majumba.

“Kufanya kazi hii bila leseni  ni kosa kisheria kanuni inaelekeza kwamba atachukuliwa hatua anafanyakazi ya utandazaji  umeme bila ya kuwa kibali cha EWURA  atatozwa faini, kupewa kifungo na adhabu zote mbili kwa pamoja inategemea na kosa,”amesema. 

Naye Katibu wa  Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), Suleiman Msuya aliishukuru EWURA kwa mafunzo hayo huku akitoa rai kwa waandishi wa habari kutumia elimu walioipata kutoa taarifa za nishati na maji kwa usahihi zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here