Home KITAIFA BoT YAJA NA MFUMO WA KIDIGITALI WA MALALAMIKO

BoT YAJA NA MFUMO WA KIDIGITALI WA MALALAMIKO

Dar es Salaam

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) inatarajia kuzindua mfumo wa kidigitali wa utatuzi wa Malalamiko ya wananchi(FCRS), utakaomwezesha mtumiaji wa huduma za kifedha kuwasilisha malalamiko kutumia mtandao, kuanzia Januari mwaka 2025.

Hayo yamesemwa leo Disemba,10 2024 Jijini Dar es Salaam, Kaimi Mkurugenzi wa Huduma Jumuishi za Fedha wa BoT, Nangi Massawe wakati akifungua warsha ya siku mbili kuhusu mfumo wa malalamiko kwa wawakilishi wa taasisi za fedha nchini amesema mfumo umekamilika kinachofanyika sasa ni kutoa elimu kwa taasisi za fedha kuuelewa kwani wao ndio wanaokutana na wateja.

Amesema jukumu kubwa la benki kuu ni kuhakikisha linamlinda mtumiaji wa huduma za kifedha kuwa na uelewa wa masuala ya kifedha, kujua ni wapi atawasilisha malalamiko yake na kupata haki, kani wamekuwa wakifanya hivyo kujenga imani na huduma za kifedha na kutumia huduma rasmi kukamilisha lengo la kuwepo kwa huduma jumuishi.

“Mfumo umetengenezwa na kukamilika, tunaamini ifikapo Januari katikati, tutauzindua rasmi wananchi waweze kutuma malalamiko yao, ni muhimu sana kuulewa kupitia warsha hii, tuuelewa vizuri na kuanza kuutumia kabla ya kuuzindua, kwa sababu tutahakikisha kama kuna tatizo, mteja anafikisha kwa haraka na linafika kwa haraka na kupata haki yake kwa haraka,” amesema.

Naye Kaimu Meneja wa Kumlinda Mtumiaji wa Huduma za Kifedha, Dk. Hadija Kishimba,
alisema lengo la BoT, kuandaa warsha hiyo kwa taasisi za fedha ni kuuelewa mfumo, kwani wao ndiyo wanaokutana na wateja.

Amewataka watumie mfumo huo kwa sababu unakwenda kusogeza huduma kwa mwananchi kwani wanataka alalamike kupitia mtandao kwa njia ya kompyuta.

Amesema lengo la BoT, ni kutafuta namna bora ya kutumia teknolojia kuwafikia wananchi katika kuwapa huduma, kwani jukumu la benki hiyo ni kuongeza fedha jumuishi nchini, hvyo kumekuwa na changamoto ya kuongeza imani mtu akipata tatizo apate ufumbuzi wa haraka.

Amesema kwa sasa wanapokea malalamiko kupitia matawi yao na dawati ya malamiko kupitia njia ya barua pepe, simu au kuandika barua na kufikisha hivyo, waona njia hiyo inaweza kutowafikisha zaidi ya teknolojia.

“Tukaona tutumie mfumo kwa njia ya teknolojia, mwananchi wetu asiweze kutembea katika tawi letu kutufuata, akiwa sehemu yake ya kazi anaweza kuandika lalamiko lake na kuweza kusaidiwa moja kwa moja na tumefanya hivyo kwa sababu wananchi wengi wanapenda kutumia huduma za fedha lakini kutishwa na mazingira ambayo akifika anaweza asifikishe taarifa zake vizuri,” amesema.

Pia, kuwasaidia kuwa na imani na sekta za fedha kwa sababu mbeleni wana malengo ufike katika mkono wa mwananchi kurahisisha upatikanaji wa haki na mwanachi akitaka kulalamika aanze na taasisi yake ya kifedha na asiporidhika atakapotumia mfumo tutamuuliza taasisi aliyotumia na kumsaidia.

“Kiutaratibu huwa tunapimwa kidunia na huwa kuna vitu wanaviangalia kwa sababu ukisema fedha jumuishi kuwa tunaangalia vitu vitatu ikiwa umeizungumzia huduma, ninatumia huduma, ubora wa huduma,”amesema.

Kwa upande wake, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa bebki ya NMB, Elizabeth Mhina amesema wamefurahi BoT kuweka mfumo kuwa wa moja kwa moja hivyo itawasaidia kurahisisha kazi na kuwafikia wateja na Watanzania kwa ujumla.

“Yapo malalamiko mengi wamekuwa wakiyapokea kikubwa ni changamoto ya elimu kwa wateja kwa mfano kuibiwa fedha katika ATM na kadi wamekuwa wakiyapata kila siku, ni suala la elimu kuwa wasitoe namba za siri, bado tunatoa elimu kuwafikia wateja wetu kudhibiti wizi,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here