Dar es salaam
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dar es Salaam imeendelea kutoa mafunzo kwa vitendo na ubunifu zaidi ili kuleta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili jamii ikiwemo malaria fangasi
Akizungumza leo Desemba 02, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tisa la ya Sayansi Meneja Uhusiano kwa Umma Veta, Sitta Peter, amesema katika kipindi cha miaka ΕΊ mitano kimefanikiwa kuibua bunifu 118 na kati ya hizo 13 zimeingizwa sokoni na 45 zipo katika mchakato wa kuingizwa sokoni.
Sita amebainisha kuwa katika maonyesho hayo wamekuja bunifu za kupunguza mbu.anayeeneza. Malaria ambapo zipo dawa za pia fangasi, UTI na ya hivyo ni yvema Watanzania analaribishwa kutembelea banda la maonyesho na kununua dawa ili kuwaongezea hamasa za kuendelea kubuni dawa nyingine.
“Leo tupo katika maonesho haya ili ya 9 tukiwa na bidhaa hizi muhimu kuwaonesha watanzania na jamii kwa ujumla na ambavyo tumeweza kufanikiwa katika kutoa mafunzo kwa wanafunzi na kubuni bidhaa ambazo ni msaada mkubwa kwa jamii katika mapambano dhidi ya Malaria,fangasi na UTI” amesema Sitta
Naye Mwalimu wa Chuo cha VETA, Alli Issa ambaye amesema kutokana na kufanikiwa kubuni bidhaa mbalimbali wa tayari wamezipatia hati miliki ili bunifu hizo zisiweze kuchukuliwa au kuigwa na wengine na bidhaa ambazo bado hatujaziingiza sokoni wanaendelea na mchakato wa kupata miliki bunifu.
Naye Mvumbuzi wa kifaa cha kufundushia mfumo wa jua na muundo wa Atomu, Ernest Maranya, amesema tayari kifaa hicho kimepata ruhusa ya kufundishia kwenye shule za msingi na sekondari baada ya kupata Ithibatia kutoka Wizara ya Elimu.
Kutokana na hilo, Maranya ambaye pia amewahi kuwa mwanafunzi hicho, ametoa ombi kwa Serikali na wadau wa elimu kumsaidia mtaji ili aweze kutengeneza vifaa vingine kwa wingi jambo ambalo litakalosaidia mlengo aliokusudia kwa.kupelekwa kwenye shule mbalimbali nchini.
“Nimefanya kazi kubwa Katika kubuni kifaa hiki na ninaamini wanafunzi wengi wataweza kuelewa vizuri somo la mifumo ya jua, hivyo naomba wa elimu waniwezeshe mtaji ili niweze kutengeneza kifaa hiki kwa wingi, kwanj natamani kufanya bunifu nyingi lakini raslimali fedha ni changamoto kubwa inayonikabili,” amesema Maranya