Dar es Salaam
MKURUGENZI Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi amesisitiza kuwa katika kipindi cha uongozi wake atahakikisha watumishi wanapata stahiki zao kwa wakati ili kuepuka malimbikizo ya madeni.
Profesa Janabi amesema hayo leo Novemba, 29 2024 jijini Dar es Salaam kwenye kikao cha 29 cha Baraza la Wafanyakazi la MNH kinachofanyika Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kufanya hivyo ni kutambua umuhimu wa kazi wanazozifanya.
“Baada ya uhakiki wa madeni ya watumishi tayari hospitali imeshalipa zaidi ya asilimia 50 ya madeni hayo na kuwahakikishia watumishi kuwa uongozi utaendelea kulipa madeni kwa awamu,” ameongeza Profesa Janabi
Amesema pamoja na kulipa madeni ya watumishi hospitali pia imeweka mkakati wa kulipa madeni ya wazabuni kwakuwa wana mchango mkubwa katika kuhakikisha huduma zinaendelea kutolewa bila kuathiri ubora wa huduma hizo.