Home KITAIFA ELIMU YA USAFIRISHAJI WA KEMIKALI BADO NI MUHIMU KWA WATANZANIA

ELIMU YA USAFIRISHAJI WA KEMIKALI BADO NI MUHIMU KWA WATANZANIA

Dodoma

IMEELEZWA kuwa sekta binafsi bado inachangamoto kwenye utoaji wa elimu kwa Wafanyakazi wao na jamii inayowazunguka juu ya madhara ya kemikali na hatua zinazotakiwa j ya kuepuka madhara hayo yasitokee.

Hayo aliyabainisha leo Novemba, 23 2024 jijini Dodoma,Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), George Ķatabazi wakati akihitimisha kampeni ya utoaji elimu kwa umma juu ya usafirishaji Salama wa kemikali hatarishi ya sodiam sayanaidi.

Amesema asilimia kubwa ya watanzania wengi bado hawana elimu ya kutosha juu ya madhara ya kemikali hiyo.

Amesema matumizi na faida nyingi za kemikali ni nyingi na hazina mbadala katika maisha ya kila siku ya wanadamu na wanaona kemikali zinatumika katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, kilimo, viwanda, maji na madini.

“Sekta binafsi bado ni changamoto kutoa elimu kwa umma hivyo kampuni chache zinatoa elimu na zipongeza hivyo kuna kampuni hazitekelezi twaka la hili la kisheria na leo hazipo zichukuliwe hatua,” amesema Katabazi.

Alisema kuwa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za viwanda na majumbani Na. 3 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2020 zilitungwa kwa lengo la kulinda afya na mazingira.

Aidha amesema katika utekelezaji wake wa sheria na kanuni hizo ziliweka mashariti mbalimbali ili kuwezesha kemikali hizo kuendelea kuingia nchini kuhifadhiwa, kusafirisha na kutumiwa bila kuleta madhara kwa afya na mazingira.

“Mojawapo ya mashariti ya msingi katika utekelezaji wa sheria hii ni utoaji elimu kwa makundi mbalimbali ya wafanyakazi mahala pa kazi na jamii ambayo inakuwa kwenye hali hatarishi ya kemikali hizi hususan wakati wa usafirishaji na shariti hili la kutoa elimu linapaswa kutekelezwa naa serikali na sekta binafsi,”ameeleza.

Amesema kuwa pamoja na madhara makubwa ya kemikali hizo kwa afya na mazingira kemikali hizo ni muhimu katika uchumi wa nchi na uchumi wa mtu mmoja mmoja na zinazotumika katika shughuli mbalimbali ikiwemo uchenjuaji na upatikanaji wa dhahabu.

Katabazi amewaomba kuendelea kutoa elimu hiyo kuwa lengo ni kuboresha usalama kwa wananchi na waliopata elimu wakawe mabalozi wazuri.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti na Usimamizi wa Kemikali Nchini Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ( GCLA), Daniel Ndiyo amesema wamekutana na wadau mbalimbali kusimamia usalama wa kemikali kwasababu kemikali zinaingia kwa wingi nchi na zinahitajika kwaajili ya shughuli mbalimbali.

“Mamlaka hii imekuwa ikitoa mafunzo ya mara kwa mara kwa makundi mbalimbali ikiwa pamoja na wajasiriamali wadogo, wachimbaji wa dhahabu wasimamizi wa kemikali mahala pa kazi madereva wanaosafirisha kemikali na jamii kwa ujumla,” amesema

Kwa upande wake kiongozi wa usafirishaji wa Kampuni ya Barricki, Joseph Mbanga amesema walikuwa wakipata ushirikiano mkubwa tangu kuanza kwa kampeni hiyo.

“Msafirishaji na polisi wamekuwa wanashirikia na Jeshi la polisi kuanzia mwanzo wa Safari hadi mwisho wa safari elimu hii imetusaidia sana ,”amesema.

Kampeni hiyo ilizunduliwa Novemba, 14 jijini Dar es Salaam na kuhitimishwa leo Novemba 23 jijini Dodoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here