Home KITAIFA AWESO ATAMBUA MCHANGO WA MAKAMPUNI YA CHINA KATIKA UTEJELEZAJI MIRADI YA MAJI

AWESO ATAMBUA MCHANGO WA MAKAMPUNI YA CHINA KATIKA UTEJELEZAJI MIRADI YA MAJI

Dar es Salaam

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ameyapongeza makampuni ya Ujenzi ya China kwa kazi kubwa ya utekelezaji na ujenzi wa Miradi mingi mikubwa ya Kitaifa hususani miradi ya Maji.

Waziri Aweso ameyasema hayo leo Novemba,14 2024 katika ukumbi wa Johari Rotana jijini Dar es Salaam alipokua akitoa hotuba yake alipoalikwa katika miaka 20 ya kampuni kutoka China ya Beijing Construction Engeneering Group(BCEG).

Katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi amekua ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, Waziri Aweso amesisitiza juu ya mashirikiano ya kihistoria kati ya Nchi ya Tanzania na China na faida yake katika maendeleo makubwa ya Taifa la Tanzania hususani katika ujenzi wa Miundombinu.

Waziri Aweso ameahidi Wizara ya Maji kuendelea kutoa ushirikiano na makampuni ya China katika ujenzi na utekelezaji wa Miradi ya Maji kwani kazi yao ni nzuri na yenye kuonekana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here