Home KITAIFA BoT – ITAENDELEA KUHAKIKISHA SEKTA YA FEDHA INAKUWA THABITI, IMARA NA...

BoT – ITAENDELEA KUHAKIKISHA SEKTA YA FEDHA INAKUWA THABITI, IMARA NA STAHIMILIVU

Dar es Salaam

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema ikiwa na jukumu la kusimamia taasisi za fedha itaendelea kuhakikisha sekta ya fedha inakuwa thabiti, imara na stahimilivu ili kuwawezesha shughuli za uchumi zinapatikana kwa wakati.

Kaim Meneja Huduma Ndogo za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dickson Gama

Akizungumza leo Novemba, 14 2024 jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja Huduma Ndogo za Fedha, Dickson Gama wakati akifungua mafunzo kwa wahariri na waandishi wa habari kuhusu usimamizi wa mikopo ya mitandaoni.

Amesema Banki Kuu imeandaa semina hiyo kwa wahariri na waandishi wa habari lengo ni kujenga uelewa mzuri zaidi.

“Ni jukumu la BoT katika kusimamia huduma Ndogo za fedha nchini hivyo kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari kiunganishi kati ya Benki Kuu na jamii ya watanzania na dunia kwa ujumla,”amesema.

Amesema semina hiyo ina umuhimu mkubwa kutokana na ongezeko la huduma za utoaji mikopo mitandaoni pamoja na cha zake.

Gama amesema katika utekelezaji wa sheria na kanuni za huduma ndogo za fedha ni jukumu lao kama wasimamizi wa sekta hiyo.

Ameeleza kuwa mikopo ya mitandaoni imekuwa ni sehemu ya mfumo wa fedha kwani imerahisisha utoaji wa huduma za mikopo kwa urahisi zaidi na haraka.

Amesema ukuaji huo wa haraka umesababisha changamoto kadhaa ikiwemo masuala ya kimaadiki, riba kubwa gharama kubwa za mikopo na kukosekana kwa taarifa.

Gama amesema kutokana na changamoto hizo wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu ili kufanya huduma hiyo kuwa na manufaa kwa wananchi na mtoa huduma kuidhinishwa na BoT.

Kwa upande wake, Meneja Msaidizi wa Huduma Ndogo za Fedha BoT, Mary Ngassa amesema kufuatia changamoto ya ukiukwaji sheria katika utoaji wa mikopo kidigitali.

Amesema Benki Kuu imetoa mwongozo kwa watoa huduma ndogo za fedha wa daraja la pili wanatoa huduma za mikopo kwa njia ya kidigitali wa mwaka 2024.

“Kifungu Na 3.0 cha mwongozo huu kimewataka watoa mikopo hawa pamoja na mengine kuwa na leseni na kutunza faragha,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here