Dar es Salaam
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC), Kaimu Mkeyenge amesema wananchi wa Tanzania wana uelewa wa asilimia mbili tu kuhusu elimu ya bima huku lengo ni kufikia asilimia tano kama ilivyo nchi zingine
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC), Kaimu Mkeyenge
Hayo ameyabainisha leo Novemba, 12 2024 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi huyo wakati akizindua kampeni ya NIC Kitaa amesema lengo ni kutoa elimu ya bima kwa watanzania waelewe faida na muhimu.
“Uelewa wa bima bado uko chini sisi kama Taasisi kongwe ya serikali tunawajibu wa kusaidia serikali kwa sababu bima ni ukusanyaji wa fedha za wananchi ambao wanahisi wakipata majanga wasaidiwe na faida yake inaweza kusaidia uchumi ambao unawekezwa katika mabenki mbalimbali hivyo tunaongeza mtaji kwenye soko hususan sekta ya bima,”amesema Mkeyenge.
Amesema wanaoingia msimu wa pili wa kampeni wa NIC Kitaa kusogeza huduma kwa wananchi na kuhakikisha elimu ya bima inawafikia wote na kutambua umuhimu wa bima.
Mkeyenge amesema kutoa elimu hiyo ni kuendeleza sera ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya bima kwa wote na kuhakikisha watanzania wote wanatumia bima.
Ameeleza kuwa kampeni hiyo itafanyika nchi nzima ili kuwafikia wananchi kupata elimu hiyo.kwa sasa wameanza na mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Singida.
Ameongeza kuwa pamoja na kutoa elimu ya kampeni hiyo wataambatisha na kuandikisha bima kwa wateja wapya na kulipa madeni sio lazima waje ofisini wamewasogezea huduma.