Na Saidina Msangi, Dodoma
Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo na Waziri wa Madini Antony Mavunde wamekutana na kufanya mazungumzo jijini Dodoma kuhusu maendeleo ya Sekta ya madini na uwekezaji ili kuendelea kukuza Uchumi wa nchi.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Japhet Justine na wajumbe wengine kutoka Wizara hizo tatu.