Zanzibar
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah amekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 75 iliyotolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ikiwa ni Programu ya mikopo kwa Makundi Maalum Wanawake,Vijana na Walema na kueleza kuwa kazi ya Serikali ya Awamu ya Naneni kuwatumikia Wazanzibari hasa katika kuwaletea maendeleo wananchi kupitia Nyanja mbali mbali za kiuchumi na kijamii.
Makamu wa Pili wa Rais Hemed amefanya makabidhiano hayo Oktoba, 31 2024 Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati wa Kongamano lililoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Jumuiya ya CCM la kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa uongozi wake wenye mafanikio makubwa
Amesema katika kipindi cha Miaka Minne baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa UWT Zainab Khamis Shomari (MNEC) kuhusiana na manufaa mbalimbali wanayoyapata Wananchi haswa Wanawake katika uongozi wa Rais Dk.Mwinyi.
“Serikali itaendela kuwafikia na kuwawezesha wajasiriamali wote nchini ili waweze kufanya kazi zao katika mazingira mazuri na kukuza mitaji ya biashara zao kwa faida yao binafsi na Taifa kwa ujumla,Mikopo hii ni miongoni mwa kazi kubwa inayofanywa na Rais Dk. Mwinyi ya kuwaletea wananchi maendeleo,na Jumuiya ya UWT imekuwa sauti ya wananchi na Wanawake katika kuzifikisha changamoto za wananchi kwa viongozi,”amesema.
Hemed amesema miradi mbali mbali inayoendelea kujengwa na Serikali kwa Unguja na Pemba ambayo imemgusa kila mwanachi wa Zanzibar hivyo ipo haja na hoja ya kuendelea kuyatangaza mazuri yanayofanywa na viongozi wakuu wa nchi.
Naye Makamu Mwenyekiti wa UWT, Zainab Khamis Shomari amesema Utekelezaji wa Ilani katika kipengele cha kuwawezesha wanawake kimetekelezwa kwa kiasi kikubwa ambapo wanawake wamekuwa wakinufaika kupitia program mbali mbali zinazotekelezwa na Serikali za kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Amesema UWT imejipanga kuwafikia na kuwawezesha wanawake wengi wa Zanzibar kwa kuwapatia mikopo yenyenye Thamani ya Shilingi Milioni 75 zitakazotolewa kwa wanawake wa Mkoa wa kaskazini Pemba ambapo Milioni 170 zitatolewa kwa Pemba nzima
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa UWT , Suzan Peter Kunmabi (MNEC) amesema Serikali ya Awamu ya nane imefanya mambo mengi ambayo yanawanufaisha wanawake katika nyanja mbali mbali za kiuchumi na kijamii ndani ya Zanzibar.
Katibu Mkuu Suzan amesema wanawake wa UWT watahakikisha kwa namna yoyote ile Rais Dk. Mwinyi anapata kura nyingi za heshima zitakazomuwezesha kuendelea kuiongoza Zanzibar na kuwaletea maendeleo wananchi wake kwa miaka mitamo ijayo.
Ameiomba Serikali kuendelea kuwatumia wataalamu wanawake katika harakati mbali mbali za Chama na Serikalini ikiwemo kuwapa nafasi na kuwaamini katika kusimamia miradi ya maendele inayoendelea kujengwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali za kuwawezesha wanawake kiuchumi.