Dodoma
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amewataka Watumishi wote wa wizara hiyo pamoja na vyombo vyake vya usalama vilipovyo chini ya Wizara hiyo kuzingatia falsafa ya 4R za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni pamoja na kukubali Mabadiliko yenye tija ya kiutendaji kwa maslahi mapana ya nchi.
Waziri Masauni ameyasema hayo lwakati akifungua Kikao cha Mwaka cha Watumishi wa Wizara hiyo, kilichofanyika jijini Dodoma, Oktoba 29, 2024.
Mhandisi Masauni amesema Watumishi wasiogope kufanya mabadiliko pale inapohitajika kufanya hivyo.
“Kwenye vyombo kuna mabadiliko ambayo tumeyafanya ambapo mwanzo waliyaona ni magumu lakini yameoneka kuleta tija kwa Vyombo hivyo,”amesema Mhandisi Masauni.
Katika hatua nyingine amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kuboresha mazingira ya utendaji wa Wizara hiyo na vyombo vyake vya Usalama, ikiwemo kuongeza bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024.