Home KITAIFA PROFESA IKINGURA AONGOZA KIKAO CHA 20 BODI YA GST

PROFESA IKINGURA AONGOZA KIKAO CHA 20 BODI YA GST

Asisitiza juhudi na ubunifu kazini

Dodoma

MWENYEKITI wa Bodi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Profesa Justinian Ikingura ameongoza Kikao cha 20 cha Bodi ya Taasisi hiyo ambapo ameitaka Menejimenti ya GST kuongeza juhudi na ubunifu katika ukusanyaji wa maduhuli ili kufikia lengo lililowekwa na Serikali.

Hayo ameyasema leo Oktoba 24, 2024 katika kikao cha Bodi ya GST kilichofanyika kwenye ukumbi wa Profesa Abdulkarim Mruma uliyopo Jijini Dodoma ambapo wajumbe wa Bodi hiyo na Menejimenti ya GST wameshiriki.

Aidha, Profesa Ikingura amesisitiza kuhakikisha ukusanyaji wa sampuli za miamba za kuhifadhiwa katika Makumbusho ya Jiolojia (Geological Museum) unafanyika wakati wa ugani na kuweka mwongozo wa namna bora ya ukusanyaji wa sampuli hizo.

Katika hatua nyingine, Profes Ikingura ameielekeza Menejimenti ya GST kuhakikisha inatangaza kwa Umma matokeo na umuhimu wa tafiti zinazofanywa katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuufahamisha Umma.

Pamoja na mambo mengine, ameipongeza GST kwa kuendelea kumiliki Ithibati ya Ubora katika utoaji huduma za Maabara iliyoipata Mwaka 2015 baada ya kukidhi viwango vya Kimataifa vya utoaji wa huduma za Maabara.

Pia, Profesa ameielekeza Menejimenti ya GST kuendelea kufuatilia upatikanaji wa Ithibati ya Vyungu vya kuyeyushia sampuli za madini ya dhahabu ili kuwaridhisha na kuwahakikishia watumiaji wa bidhaa hiyo.

Vikao vya Bodi ya GST hufanyika mara nne kwa Mwaka ambapo ni kila baada ya kila robo ya kila Mwaka wa Fedha ambapo Kikao cha 20 chia Bodi hiyo kimelenga kujadili taarifa ya Utekelezaji wa GST kwa kipindi cha kuanzia Julai hadi Septemba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here