Home KITAIFA WANAFUNZI 1,633,900 KUANZA MTIHANI DARASA LA NNE LEO.

WANAFUNZI 1,633,900 KUANZA MTIHANI DARASA LA NNE LEO.

Dar es Salaam

JUMLA ya wanafunzi 1,633,900 waliopo katika shule za msingi 20,069 Tanzania Bara wamesajiliwa kufanya mtihani wa upimaji wa Kitaifa wa darasa la nne unaotarajiwa kuanza leo.

Pia wanafunzi 879,291 waliopo katika shule za sekondari 6,617 zilizopo Tanzania Bara wanatarajiwa kuanza mtihani wa Kitaifa wa kidato cha pili unaotarajia kuanza Oktoba 28 hadi Novemba saba mwaka huu.

Akizungumza Oktoba, 22 2024 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Dk.Said Mohamed amesema jumla ya wanafunzi 1,633,900 wamesajiliwa kufanya upimaji wa
kitaifa wa darasa la nne, 2024.

“Kati yao wavulana ni 794,021 sawa na asilimia 48.60 na wasichana ni 839,879 sawa na asilimia
51.40.

“Kati ya wanafunzi 1,633,900 waliosajiliwa kufanya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne mwaka 2024, wanafunzi 1,532,421 sawa na asilimia 93.79 watafanya upimaji kwa lugha ya Kiswahili na wanafunzi 101,479 sawa na asilimia 6.21 watafanya Upimaji kwa lugha ya Kiingereza ambayo wamekuwa wakiitumia katika kujifunzia,”amesema Dk.Mohamed.

Amesema wapo pia wanafunzi 5,938 wenye mahitaji maalum kati yao wenye uoni hafifu ni 1,185 wasioona 132,wenye uziwi 1,178 ,wenye ulemavu wa akili 1,800 na wenye ulemavu wa viungp ni 1,643.

Akizungumzia kuhusu wanafunzi wa kidato cha pili Dk.Mohamed amesema jumla ya wanafunzi 879,291 wamesajiliwa kufanya upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili, 2024.

“Kati yao 869,673 ni wanafunzi wa shule na 9,618 ni wanafunzi wa Kujitegemea,kati ya wanafunzi wa shule 869,673 waliosajiliwa,wavulana ni 399,383 sawa na asilimia 45.92 na wasichana ni 470,290 sawa na asilimia 54.08.

“Aidha, wapo wanafunzi 1,863 wenye mahitaji maalum kati yao, wenye uoni hafifu ni 1,053, wasioona ni 83, wenye uziwi 540, wenye ulemavu wa viungo 137 na wenye ulemavu wa akili 50,”amesema Dk.Mohamed.

Amesema upande wa wanafunzi wa kujitegemea 9,618 waliosajiliwa, wavulana ni 3,712 sawa na asilimia 38.59 na wasichana ni 5,906 sawa na asilimia 61.41.

Amesema wapo pia wanafunzi 66 wenye mahitaji maalum kati yao, wenye uoni hafifu ni 65 na asiyeona mmoja.

Amesema maandalizi yote kwa ajili ya upimaji wa darasa la nne na kidato cha pilo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa karatasi za upimaji
pamoja na nyaraka zote muhimu zinazohusu upimaji huo katika Halmashauri/Manispaa zote nchini.

Ameongeza kuwa maandalizi yote kwa ajilli ya wanafunzi wenye mahitaji maalum pia yamefanyika ipasavyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here