Home KITAIFA TANZANIA NA IRAN ZA SAINI HATI 11 ZA MAKUBALIANO KIBIASHARA

TANZANIA NA IRAN ZA SAINI HATI 11 ZA MAKUBALIANO KIBIASHARA

Dar es Salaam

SERIKALI ya Tanzania na Jamhuri ya Kiislam ya Iran zimesaini hati 11 za makubaliano ya kibiashara ambapo sita ni baina ya serikali na mitano ni ya sekta binafsi lengo likiwa kukuza diplomasia na uchumi katika nchi hizo.

Akizungumza Oktoba 19,2024 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo mara baada ya kushuhudia utiaji wa saini katika mikataba katika ufunguzi wa mkutano wa tano wa tume ya pamoja ya kudumu (JPC) alisema hiyo ni fursa kwa nchi kwani ushirikiano huo utachochea ukuaji wa uchumi lakini pia kuboresha sekta mbalimbali katika nchi.

Alisema kufikia kwa makubaliano hayo ni matokea mazuri na hitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha nchi inapanuka na uchumi unakua.

“Kipekee niwashukuru Marais wa nchi hizi mbili kwa kuimarisha ushirikiano wa uwili na azma ya kuongeA maeneo ya ushirikiano iliwemo biashara na uwekezaji, kilimo, nishati,ulinzi na usalama na elimu,” alisema balozi Kombo.

Pia aliwataka watanzania wanaojihusisha na biashara ikiwemo Chemba ya biashara na Tantrade kuchangamkia fursa hizo pindi zinapojitokeza ili kuendelea kuimarisha uchumi.

Aliongeza kuwa maeneo mengine ambayo Tanzania na Iran yatahusisha sekta ya afya,sayansi na teknolojia pamoja na utamaduni.

Kwa upande wake Waziri wa kilimo wa Jamuhuri ya kiislam ya Iran Golamreza Nouri Ghezelcheh amesema ushirikiano huu ambao wameingia katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo utaenda kuzisaidia nchi zote mbili katika buboresha shughuli zao za kilimo kwa maslah ya wananchi na nchinyenyewe.

“Marais wa pande zote wanasisitiza juu ya maendeleo ya uhusiano wa Afrika hivyo ni matumaini yangu kwamba kutiwa saini kwa hati hizi za ushirikiano utaleta uhusiano mzuri zaidi katika awamu mpya”,alisema Nouri Ghezelcheh.

Hafla ya kusaini hati hizo za makubaliano imefanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere (JNICC)jijini Dar es salaam katika mkutano wa pamoja wa kudumu ya ushirikiano baina ya Tanzania na Iran.

Aidha uwekaji wa saini hizo umehusisha wizara za kisekta,baadhi ya taasisi za umma na Taasisi binafsi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here