Dar es Salaam
KAMPUNI ya Kili MediAir Nchini imesema inaendelea kuboresha huduma pamoja na kutoa huduma ya Uokozi kwa watalii pia inafanya utalii wa anga ili watalii na watanzania kufurahia huduma.
Akizungumza leo Oktoba 12, 2024, Daktari wa Uokozi wa Kampuni hiyo, Jimmy Daniel kwenye maonyesho ya nane ya S!TE yanayoendelea katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam alisema kampuni hiyo imetimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake.
Amesema kampuni hiyo inajishughulisha na usalama wa watalii katika vivutio na kwa sasa imejikita zaidi Kaskazini huku wakiwa na malengo ya kufikia vivutio vyote nchini.
“Lakini nje ya hapo tumejidhatiti sasa hivi tumetengeza wigo kwamba hatufanyi tu uokozi bali Utalii wa anga. Kwamba tunakutana na watu wanatamani kuweza kufanya utalii mfano katika Mlima Kilimanjaro lakini kwaajili ya umri au maradhi wanashindwa,” amesema.
Amesema moja ya changamoto wanayokabiliana nayo ni watu wengi wanajua kuwa huduma yao ni uokozi tu hivyo wanaendelea kutoa elimu wananchi kuwa wanafanya na utalii wa anga.
Aidha amesema kampuni hiyo inakabiiwa na changamoto kubwa watu wengi wanajua kuwa huduma yao ni moja ya uokozi kuna huduma zingine zinazotolewa nawanaendelea kutoa elimu wananchi watambue huduma zinazotolewa na kampuni hiyo.
Pia amesema Changamoto ni kuwahudumia watu wote na watalii ambao wana bima ya afya wanaweza kutumia katika kuwasaidia kuna wakati wanakutana na watu wenye shida ya uchumi ambao wanapanda milima na wanaobeba mizigo wakipata changamoto wao wanajitahidi kujitolea.Kama watanzania kuokoa bila kuangalia gharama pamoja na vitu vingine.
Amesema hawahusiki tuu na suala la uokozi na wajitahi kuongeza huduma ikiwemo utalii wa anga.
“Sisi tunajihusisha na wokozi kwa njia ya anga kwa kutumia helkopta pia kwa njia ya ardhini,” amesema Dk. Jimmy.