Home KITAIFA WATU 11 WAMESHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA MBALIMBALI

WATU 11 WAMESHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA MBALIMBALI

Dar es Salaam

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa 11 kwa vitendo vya kihalifu ikiwa ni katika kuendelea kusimamia mkakati wa kuzuia vitendo vya kihalifu na kuhakikisha Dar es Salaam inaendelea kuwa salama.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Oktoba, 3 2024 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Muliro Jumanne Muliro amesema Jeshi limekuwa linafanya ufuatiliaji mkali mwezi Septemba 2024 na kufanikiwa kumkamata watuhumiwa hao.

Amewataka watuhumiwa kuwa ni TWAHA SALUM miaka 53 na wenzake Saba kwa tuhuma za hujuma ya kuharibu miundombinu ya bomba la gas la kampuni ya  ORYX  linalosafirisha Gas kutoka Bandari ya Dar es Salaam ambapo wamehojiwa kwa kina, ushahidi umekusanywa na watafikishwa kwenye mamlaka zingine kwa hatua zaidi za kisheria.

Aidha katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linamshikilia Daud Matola dereva, miaka 50 mkazi wa Kimara Dar es Salaam na wenzake wawili kwa tuhuma za wizi wa madini aina ya Copper cathode yaliyokuwa yakisafirishwa kutoka nchini Congo kwenda  Bandari ya Dar es salaam.

Amesema tukio hilo lilitokea mnamo Agost,7 2024 huku mtuhumiwa dereva na wenzake  wakiwa na gari namba  T. 882 DQK aina ya Benz na Tela T.884 EEE Mali ya kampuni ya FAA Trucks walituhumiwa kutenda kosa hilo ambapo baada ya wizi huo, watuhumiwa walilitelekeza  gari hilo jijini Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linatoa wito kwa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa na kuahidi kutokuwa na huruma kwa wahalifu na kuendelea kuwashughulikia vikali kwa mujibu wa sheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here