Home MICHEZO DK.STERGOMENA AKABIDHIWA JEZI YA TIMU YA MASHUJAA FC

DK.STERGOMENA AKABIDHIWA JEZI YA TIMU YA MASHUJAA FC

Dar es Salaam

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Stergomena Lawrence Tax Oktoba, 2 2024 amekabidhiwa jezi ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania maarufu kama Mashujaa.

Hafla hiyo fupi ya kumkabidhi Jezi Waziri imefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya Ulinzi na JKT, Upanga Jijini Dar es Salaam, ambapo imekabidhiwa jezi hiyo na Mwenyekiti wa Mashujaa FC, Kanali Benjamin Kisinda ikiwa ni kutambua mchango wa Dk. Stergomena katika kukuza na kuendeleza sekta ya michezo katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na timu ya Wizara ya Ulinzi kwa ujumla.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi ya kukabidhiwa jezi, Dk. Stergomena amewataka Timu ya Mashujaa pamoja na Timu zote zilizo chini ya Wizara na JWTZ kuhakikisha zinaendelea kushindana na kushinda ili kufikia malengo ya Wizara na Taifa kwa ujumla na akawakumbusha kuwa michezo ni Afya, Burudani na Ajira pamoja na kuimarisha afya ya akili.

Amewahakikishia wachezaji na viongozi wa Timu ya Mashujaa kuwa Wizara ipo nyuma na timu zote za Wizara kuhakikisha timu hizo zinafikia malengo yake kitaifa na kuiwakilisha nchi kimataifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here