Home MICHEZO MABINGWA WA MASHINDANO YA GOFU YA LINA PG TOUR WATEMBELEA KABURI LA...

MABINGWA WA MASHINDANO YA GOFU YA LINA PG TOUR WATEMBELEA KABURI LA MLEZI WA MAENDELEO YA GOFU YA WANAWAKE NCHINI.

Kilimanjaro

MABINGWA wa mashindano ya gofu ya Lina PG Tour wametembelea kaburi la mlezi wa maendeleo ya gofu ya wanawake nchini, marehemu Lina Nkya kwa lengo la kumuenzi na kukumbuka mazuri yote aliyoyafanya katika kukuza mchezo huo.

Ziara ya mabingwa hao wa gofu katika kaburi la mlezi huo ilifanyika Septemba 29, 2024 mara baada ya kumalizika kwa mashimo 72 ya mchezo wa raundi ya nne ya mashindano hayo yaliyofanyika katika viwanja vya klabu ya Moshi Gymkhana mkoani Kilimanjaro na kuwahusisha washindi vitengo vya gofu ya kulipwa na ridhaa kutoka vilabu vyote nchini.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo kukamilika, Mkurugenzi wa Lina PG Tour, Yasmin Chali amesema wamekuja kuzuru katika kaburi la Lina lililopo karibu na viwanja vya gofu vya klabu ya Moshi ili kuenzi kazi yake kubwa aliyoifanya katika kulea maendeleo ya gofu ya wanawake nchini.

Amesema anawashukuru nyota wa michuano na familia nzima ya gofu kwa kuitikia wito wa kushiriki michuano hiyo na kuenzi mchango wa Lina Nkya katika kuendelea gofu nchini.

“Tumekuja kuzuru kaburi lake ili kuienzi kazi yake kubwa aliyoifanya kutika kulea maendeleo ya gofu ya wanawake nchini, niwashukuru wote waliojitokeza kushiriki michuano hii ambayo inaweka alama kwa vizazi vyetu pia,” amesema Chali

Miongoni wa watu walionufaika na uongozi wa Lina Nkya ni Angel Eaton na Ayne Magombe, ambao walisema kuwa Lina ndiye alikuwa kiongozi wao wakati wakiiwakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya gofu katila ngazi ya kimataifa.

“Namkumbuka Mama Lina Nkya kwa kutuongoza vizuri wakati Tanzania iliposhika nafasi ya pili nyuma ya Afrika ya Kusini katika mashindano ya ubingwa wa Afrika nzima nchini Ghana na baadaye mwaka huohuo alituongoza kucheza mashindano ya ubingwa wa dunia nchini Argentina ambapo Tanzania pia ilifanya vizurti sana,” amesema Ayne Magombe, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa.

Angel Eaton ambaye pia aliichezea timu ya taifa kabla ya kujiunga na gofu ya kulipwa, alisema Lina Nkya ni mama wa maendeleo ya gofu kwani amehusika sana katika kukua kwa gofu ya wanawake nchini.

“Hatutamsahau Mama Nkya kwa sababu yeye ndiye haliyetuongoza sisi tufanye vizuri kimataifa. Bila yeye naamini wengi wetu tusingekuwa hapa hivi leo,” alisema Eaton ambaye ni mchezaji pekee mwanamke katika gofu ya kulipwa.

Wengine waliozuru kaburi la Lina Nkya ni Sophia Viggo ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya gofu ambapo alisema walifanya kazi kwa karibu na Mama Lina ikiwemo kuiongoza timu ya taifa ya gofu ya wanawake katika mashindano mbalimbali nje na ndani ya bara la Afrika.

“Hakika tutamkumbuka na kumuenzi daima mama Lina hasa kwa mchango wake uliopelekea gofu yetu kukua,” amesema Viggo.

Wengine waliomuenzi Lina Nkya ni Isiaka Daudi, Enosh Wanyeche, Ally Isanzu na Karim Ismail ambao waliongoza kwa gofu ya ridhaa na Nuru Mollel, Isack Wanyeche, George Sembi na Athumani Chiund ambao wamecheza vizuri katika gofu ya kulipwa.

Katika mashindano hayo ya raundi ya nne mshindi wa kwanza ni mchezaji wa gofu wa kulipwa, Nuru Mollel aliyeshinda kiasi cha Shilingi Milioni 6.8 huku mshindi wa pili akiwa Fadhil Nkya ambaye naye pia ni mchezaji wa gofu wa kulipwa aliyejipatia kiasi cha Shilingi milioni 4.3.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here