Home KITAIFA WANAKIJIJI CHA ISAGENHE WAMEUPONGEZA MTANDAO WA TECMN KWA KUFIKA KATIKA KIJIJI...

WANAKIJIJI CHA ISAGENHE WAMEUPONGEZA MTANDAO WA TECMN KWA KUFIKA KATIKA KIJIJI HICHO KUTOA ELIMU YA MASUALA YA NDOA ZA UTOTONI.

Tabora

WANAKIJIJI cha Isagenhe wilayani Nzega Vijijini,wameupongeza Mtandao wa Kutokomeza Ndoa za Utotoni(TECMN),kwa kufika katika Kijiji chao na kutoa elimu ya masuala ya ndoa za utotoni pamoja na kuangalia sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inavyowaathiri watoto.

Akizungumza Septemba, 29, 2024 Mkoani Tabora wakati wa Msafara wa TECMN ulipofika katik kijiji hicho na kutoa elimu hiyo,Kwa Upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Isagnehe,Alex Madale ametoa shukrani kwa elimu hiyo waliyopatiwa wananchi hao ili waweze kuachana na mila na desturi zilizopo.

Amesema elimu hiyo iliyotolewa itakuwa elimu tosha kwao itakayosaidia kupunguza ndoa hizo kwa watoto wakike na kuacha wasoma.

”Niwapongeze sana wanamtandao kuja na kutoa elimu,niombe wazazi wenzangu haya tunayoyasikia tufanye kazi kwa kuwatendea haki watoto wetu wa kike,”amesema.

Mwanafunzi kidato cha Tatu sekondari ya Isaghene, Gaudensia Robert amesema kuna madhara kubwa kwa wasichana kuolewa katika umri mdogo kwani wanaenda kupitia changamoto kubwa ambazo ni hatari kwao.

Amesema kuna muda wazazi wanatuambia tufanye mtihani vibaya,mfano unakuta mzazi anamwambia mtoto wake usiende shule ili uolewa anakuwa anamkataza kila siku unamkuta mtoto kuwa na huzuni mzazi anakukataza na hauna chakufanya kwahiyo unamwambia mwalimu matatizo ndipo anapokuja kuyatatua.

Mmoja wa Wazazi kutoka kijiji hicho,Riziki Hassan amesema sio lazima mtoto aolewe ndio wazazi wapate mali bali wazazi wanapaswa kuacha tama ya mali na fedha.

”Wazazi tusiwe na tamaa za Pesa kwa kuwaozesha watoto wetu wakiwa na umri mdogo bali tuhakikishe tunatafuta kwa vyanzo vingine usitegeme kupata mtoto wa kike ndio upate mali au utajiri kwa kweli hiyo ni mbaya tuache watoto wasome watimize ndoto zao,”amesema.

Kwa upande wake Mratibu wa Mtandao huo,Lilian Kimati amesema mtandao wao unamashirika 87 na umewakilishwa na Mashirika mbalimbali katika Karavan hiyo ikiwemo Shirika la Msichana Initiative,Binti Makini,Plan International, MyLegacy, Medea pamoja na Theatre Arts Femist Group ambapo wanaelekea Mkoani Tabora.

Amesema lengo la Caravan hiyo ni kupita katika mikoa minne ambayo hadi sasa wamekamilisha mikoa mitatu ambayo ni Mara,Shinyanga na huo wa Tabora ambayo ni mikoa iliyo na asilimia kubwa ya ndoa za utotoni.

”Wazazi mnapaswa kuwapeleka watoto wa kike shuleni ili waweze kusoma na kutimiza ndoto zao walizokuwa nazo,hivyo wazazi tusiwakatishe watoto wetu kwa tamaa za mali,”amesema

Naye Afisa Uchechemuzi Shirika la Msichana Initiative,Jacob Maduki amesema shirika lao limekuwa likifanya kazi na watoto katika kuwaelimisha na kuwajengea uwezo kujitambua na kuweza kupinga ukatili na ndoa za utotoni.

”Tumekuwa tukishirikisha jamii kutokana na majukwaa yao waliyotengeneza ambayo yalianza kasi mwaka 2022 yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo watoto kuelewa haki zao za msingi na sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ikitoa fursa watoto kuolewachini ya miaka 18 hasa kifungu 13 na 17,”amesema.

Amesema taasisi yao kama moja ya wanamtandao wa ,,, wamefika katika kata hiyo kwa lengo la kukusanya maoni na kuelimisha jamii dhidi ya ndoa za utotoni na kuhamasisha jamii kuweza kuwa na uelewa wa kupinga ndoa za utoto kwa kutumia sheria ya 1971 ya ndoa.

Amesema mapokeo katika programu hizo zimekuwa kubwa kutokana na jamii sasa kutambua na kutoa taarifa hasa katika majukwaa ambayo yametengenezwa na taasisi yao katika kuwaachisha watoto shule na kuwaozesha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here