Home KITAIFA RAIS DK. MWINYI: MKUTANO WA MAJAJI (SEACFJ) NI FURSA MUHIMU ZANZIBAR

RAIS DK. MWINYI: MKUTANO WA MAJAJI (SEACFJ) NI FURSA MUHIMU ZANZIBAR

Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Majaji Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika(SEACJF) unaotarjiwa kufanyika Zanzibar mwakani ni fursa muhimu ya kuimarisha ushirikiano na kuimarisha utendaji wa Mahakama kwa Nchi hizo.

Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo Aprili, 28 2025 alipozungumza na jopo la Majaji Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika waliofika Ikulu kuonana naye.

Amefafanua kuwa Mbali na kuwaleta pamoja mkutano huo itasaidia kubadilishana uzoefu baina ya nchi na nchi na Kujadili kwa pamoja changamoto za kiutendaji wa Mahakama kwa nchi wanachama.

Aidha amewahakikishia Majaji hao kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha mkutano huo wa kwanza kufanyika nchini.

Amewasisitiza Majaji hao wakati wa Mkutano huo kuvitembelea vivutio vya utalii vya Zanzibar na hatimaye kuwa Mabalozi Wazuri wa kuitangaza Zanzibar katika nchi zao hatua itayochochea kukuza sekta ya utalii inayochangia asilimia 30 ya pato la Taifa.

Naye Rais wa Jumuiya Hiyo Jaji Mkuu wa Eswatini Moses Cuthbert Maphalala amesema lengo kuu la mkutano huo ni kulinda na kuimarisha utawala wa Sheria ,Uhuru wa Mahakama , kubadilishana uzoefu pamoja na kuhakikisha mihimili ya nchi inafanya kazi kwa amoja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here