Home KITAIFA CHALAMILA : DAR NI SALAMA AELEZA MAFANIKIO NA MIPANGO YA MAENDELEO YA...

CHALAMILA : DAR NI SALAMA AELEZA MAFANIKIO NA MIPANGO YA MAENDELEO YA MKOA

-Afafanua maboresho makubwa ya miundombinu ya barabara na miradi ya kimkakati

-Awataka wananchi kuendelea kuhamasishana umuhimu wa kulipa kodi

-Awatoa hofu wananchi kuelekea uchaguzi Mkuu 2025 asema Serikali iko imara sana.

-Atoa salamu za heri ya Pasaka, asema DSM ni Salaam sana

Dar es Salaam

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila leo April 18,2025 amefafanua mambo mbalimbali ikiwemo usalama wa Mkoa, jumbe zinazozagaa juu ya mafuriko na hatua zinazochukuliwa na Serikali, Kasi ya ulipaji kodi, maboresho ya miundombinu ya barabara pamoja na nafasi ya mkoa kuelekea uchaguzi mkuu 2025.

Hayo ameyasema, Chalamila kwenye mkutano na waandishi wa Habari amesema katika kuboresha miundombinu Serikali mkoani Dar es salaam imeanza ujenzi wa daraja la jangwani mkandarasi ameanza ujenzi wa karakana ya kuhifadhia hivyo mkandarasi yupo kazini ambapo amewataka wananchi kutokuwa na shaka juu ya ujenzi huo ambao unakwenda kuwa suluhisho la mafuriko eneo hilo.

“Mpango wa ujenzi wa barabara katika mkoa huu kupitia mradi wa DMDP ambapo amesema wakandarasi wengi wameshaingia kazini na amewahakikishia wananchi kuwa barabara ambazo bado ujenzi haujaanza ndani ya muda mfupi kazi itaanza pia amesisitiza juu ya mpango wa serikali kuimarisha usafiri wa mwendokasi kupitia wawekezaji binafsi,” amesema Chalamila.

Aidha amezungumzia suala la uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwaka huu na kusisitiza kuwa licha ya tofauti za itikadi za kisiasa zilizopo Mkoa utaendelea kuwa salama kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi na kwamba kila aliejiandikisha Mkoani humo atapiga kura kwa amani na utulivu hivyo amewataka wanasiasa kufanya siasa za kistaarabu kwani Jeshi la polisi litafika kila penye viashiria vya uvunjifu wa amani.

Vilevile kupitia mkutano huo ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake kuutaarifu umma kupitia vyombo vya habari Mkuu wa Mkoa huo amezungumzia mpango wa biashara saa 24 na kusisitiza kuwa uwepo wa bandari, uwanja wa ndege wa kimataifa,kituo cha mabasi cha magufuli, umeme na soko lakimataifa la kariakoo ni nyenzo muhimu kufikia lengo la biashara saa 24.

Pia Chalamila amewatakia Kheri ya Pasaka wakristo wote na wakazi wa Dar es Salaam kwa ujumla kusherekea kwa amani na utulivu Jeshi la polisi lipo kazini saa 24.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here