Home KITAIFA ECOP YAKABIDHI CHETI CHA HAKI KIMILA YA UMILIKI WA ARDHI KWA...

ECOP YAKABIDHI CHETI CHA HAKI KIMILA YA UMILIKI WA ARDHI KWA JAMII YA AKIE

Kiteto

MRADI wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), umekabidhi cheti cha haki ya kimila ya umiliki ya ardhi ya kimila ya umiliki wa ardhi yam situ mtakatifu kwa jamii ya Akie iliyopo Kiteto mkoani Manyara ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya mradi huo iliyotolewa Mwaka 2022.

Akizungumza Aprili, 9 2025 wakati wa hafla ya kukabidhi hati hiyo iliyoambatana na uzinduzi wa zahanati sambamba na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa jamii hiyo, katika kitongojii cha Napilikunya, Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, Meneja Mkuu wa EACOP Tawi la Tanzania, Bi Wendy Brown amesema kuwa hayo ni matokeo ya ushirikiano uliopo kati ya mradi na jamii hiyo.

“Nakumbuka nilikuja hapa mwezi wa Julai mwaka 2022, wakati wa hafla ya utiliaji saini randama ya ridhaa huru ya uelewa kabla ya utekelezaji wa mradi (FPIC) ambapo mlitoa ombi maalum kwamba mnaomba ardhi yenu ya matambiko ilindwe kisheria na tulihaidi kulishughulikia, imepita miaka mitatu sasa ambapo leo tumerudi kutimiza ahadi yetu,” amesema Bi Brown.

Amesema tukio hilo ni ushahidi tosha wa namna ambayo EACOP imejipambanua kulinda na kusimamia mazingira, tamaduni pamoja na maendeleo endelevu ya jamii za pembezoni.

“EACOP inaamini maendeleo sio miundombinu pekee bali ni pamoja na mila na desturi sambamba na maisha bora, kwa kulitambua hilo, leo tutakabidhi hati ya hakimiliki ya kimila kwa familia saba ambazo ziliguswa na mradi, amesema Brown.

Aidha, Brown amesema katika wilaya ya Kiteto pekee wamewezesha upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa 875 na kati ya hivyo, vyeti 125 ni vya jamii ya Akie, mpaka kufikia sasa vyeti 112 vipo tayari na baadhi vitakabidhiwa kwa watoto wa jamii hiyo.

Amesisitiza umuhimu wa tukio hili akisema, “Makabidhiano haya yanawakilisha hatua kubwa katika dhamira yetu ya maendeleo endelevu na uwajibikaji wa kijamii. Kwa kuhakikisha umiliki wa ardhi kwa Msitu Mtakatifu wa Akie na kusaidia kaya zilizoathirika na mradi, tunathibitisha kujitolea kwetu kuheshimu urithi wa kitamaduni na kuhakikisha athari chanya kwa jamii.”

Naye Meneja wa ardhi na masuala ya kijamii Tanzania, Jean Lennock aliongeza, “Katika EACOP, tunaelewa umuhimu wa usalama wa ardhi, uhifadhi wa tamaduni, na ustawi wa kijamii. Jitihada hizi ni ushahidi wa ushirikiano wetu endelevu na jamii za wenyeji ili kuleta manufaa ya muda mrefu. Tunajivunia kuwa sehemu ya safari hii na kushuhudia mabadiliko chanya ambayo mradi unaleta katika maisha ya watu.”

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Katibu Tawala, Mufandii Msaghaa, amesema toka mradi uanze kutekelezwa, walengwa waliopitiwa na mradi huu, mbali ya kunufaika na fidia, wamekuwa wakipewa kipaumbele cha ajira hasa zile za ujuzi wa kati na ujuzi wa chini ili kujikwamua kiuchumi.

“Napilikunya ni miongoni mwa kitongoji ambacho kimenufaika na mradi, ambapo mbali ya kulipwa fidia zahanati pia ilijengwa,” amesema Msaghaa.

Ametoa rai kwa wakazi wa kiteto kueshimu maeneo waliyokabidhiwa jamii ya Akie kwani maeneo hayo si sehemu tu ya makazi bali ni maeneo wanayotumia kuabudu sambamba na kutunza kumbukumbu za tamaduni zao kwa vizazi vijavyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Jamii kutoka EACOP, Fatuma Msummi amesema mradi umekuwa ukifanya kazi kwa karibu na Serikali, (NGOS) na viongozi wa kimila katika kuhakikisha jamii za pembezoni na zilizoguswa na mradi zinanufaika.

“Hatua hizi za EACOP ni utekelezaji wa sheria na taratibu za kimataifa ambazo zinaitaka EACOP kuheshimu mila na tamaduni za watu wa asili wakati wa utekelezaji wa mradi,” amesema Msummi.

Naye Mshauri wa EACOP kuhusu vigezo vya kimataifa kwa jamii za pembezoni, Dkt. Elifuraha Laltaika amesema EACOP imekuwa ikifanya kazi kwa uwazi na kujitoa katika kuwajengea uwezo jamii.

“Toka mradi uanze kutekelezwa, walengwa waliopitiwa na mradi huu, mbali ya kunufaika na fidia, wamekuwa wakipewa kipaumbele cha ajira hasa zile za ujuzi wa kati na ujuzi wa chini ili waweze kuchangia kukuza pato la taifa,”amesema.

Yohana Lemama ambaye ni Mwenyekiti wa Jamii ya Akie, mbali ya kuipongeza EACOP kwa kueshimu tamaduni na kuthamini mila na desturi zao, amesema uwepo wa hati miliki ya ardhi utawasaidia kutunza mila na utamaduni zao kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Uwepo wa EACOP umetuwezesha sisi jamii za pembezoni kujengewa uwezo kwa kupewa mafunzo mbalimbali ikiwemo kupanda mazao kwa kutumia mbinu za kisasa za kilimo, amesema. na kuongeza kuwa uwepo wa mradi umewezesha ujenzi wa barabara, zahanati, shule na ununuzi wa madawati ya kisasa.

Wanahisa wa EACOP ni TotalEnergies yenye asilimia (62), Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) yakimiliki asilimia 15 kila moja na kampuni ya mafuta ya Kichina (CNOOC) ikiwa na asilimia nane.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here