Home KITAIFA WATU NANE WAFARIKI KWA AJALI NA WENGINE 31 MAJERUHI

WATU NANE WAFARIKI KWA AJALI NA WENGINE 31 MAJERUHI

Kilimanjaro

WATU nane wamefariki Dunia na wengine 31 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Akithibitisha Aprili, 3 2025 kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani wa Kilimanjaro, Mrakibu Msaidizi Jeremiah Mkomagi alisema kuwa, tukio hilo limetokea leo majira ya asubuhi katika barabara ya Ugweno – Mwanga.

Amesema kuwa, basi kampuni ya Mvungi lililokuwa likitokea Vuchama Ugweno kuelekea jiji Dar es salaam lilipokuwa likilikwepa gari dogo ndipo lilienda pembezoni mwa ngema ya mlima ambapo uzito uliizidi ngema na kupelekea kuanguka bondeni.

“Kama unavojua kipindi hiki ni cha mvua sasa dereva wa hili basi alikuwa analikwepa gari dogo akawa ameenda pembeni ya kingo ya mlima ndipo uzito ulipolea na kupelea kuangukia bondeni,” amesema Mkomagi.

Amesema kuwa, watu saba walifariki Dunia pale pale huku mmoja akifariki wakati anapatiwa matibabu katika hospitali ya Kanda ya KCMC na wengine 31 kujeruhiwa ambapo majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Kifula pamoja na Hospitali ya Kanda KCMC.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa hospitali ya Kanda ya KCMC, Gabriell Chiseo amethibitisha hospitali hiyo kupokea majeruhi saba ambapo wa kike ni wanne na wakiume watatu.

Chiseo amesema kuwa, kati ya majeruhi hao mmoja alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu ambaye ni mwanamke.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here