Home AFYA MOI YATOA MATIBABU YA KIBINGWA BURE KWA WANANCHI VIWANJA VYA AMANI ZANZIBAR

MOI YATOA MATIBABU YA KIBINGWA BURE KWA WANANCHI VIWANJA VYA AMANI ZANZIBAR

Zanzibar

TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) inashiriki katika kambi ya matibabu ya kibigwa na kibobezi ya mifupa, ubongo, mgongo, mishipa ya fahamu, magonjwa ya ndani na fiziotherapia kwa maofisa habari wa serikali na wananchi katika viwanja vya Amani, Zanzibar.

Kambi hiyo imeanza leo Aprili 3, 2025 ambapo wananchi na maofisa habari serikalini wamejitokeza kwa wingi kupata huduma hizo za kibingwa bure bila malipo, ikiwa ni sehemu ya kikao kazi cha 20 cha maofisa habari serikalini kinachoendelea hoteli ya New Amani, Mjini Magharibi, Zanzibar.

Akiongea na wananchi waliofika kupata huduma, daktrari bingwa mbobezi wa mifupa MOI, Dk. Tumaini Minja amesema kambi hiyo ni fursa kwa wagonjwa wa Zanzibar kupata huduma za kibingwa karibu yao ambapo wangelazimika kuzifuata jijini Dar es Salaam.

“Katika Taasisi ya MOI mtapata huduma za kibingwa za mifupa, ubongo, mgongo, mishipa ya fahamu, magonjwa ya ndani na fiziotherapia, Taasisi ya MOI imesogeza karibu huduma hizi ili kuwaondolea adha ya kusafiri hadi jijini Dar es Salaam,” amesema Dk. Minja.

“Huduma hizi ni bure, hivyo tuwaalike wananchi wenye magonjwa ya mifupa, mgongo na mishipa ya fahamu kutumia nafasi hii, wagonjwa watapatiwa huduma za ushauri na dawa,”ameongeza.

Katika kambi hiyo MOI inahusisha hospitali mwenyeji ya Lumumba, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here