Home KITAIFA DEREVA ALIYESABISHA KIFO CHA MKUU WA POLISI CHANIKA AKAMATWA MKOANI MBEYA

DEREVA ALIYESABISHA KIFO CHA MKUU WA POLISI CHANIKA AKAMATWA MKOANI MBEYA

Dar es salaam

JESHI la Polisi limefanikiwa kumkamata Dereva Elia Asule Mbugi@Dogobata Mnyakyusa(25),mkazi za Segerea aliyekuwa aliyetoroka baada ya kusababisha kifo cha SP Awadh Ramadhani aliyekuwa Mkuu wa Polisi Chanika Machi 17,2025 na gari namba T 580 EAE aina ya TATA@Dajadala aliyokuwa akiendesha siku hiyo

Mtuhumiwa huyo alikamatwa na Makachero wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Machi 27,2025 huko maeneo ya Mbalizi Mkoani Mbeya, Atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo

Akizungumza na Waandishi wa habari Leo Machi 30,2025 Jijini Dar es salaam Kamanda Jumanne Muliro amesema Jeshi la Polisi halitasita kuchukuwa hatua kali za kisheria kwa dalili za vitendo vyovyote vya kijinai au vile vya usalama barabarani kwa madereva wote wa vyombo vya moto wenye tabia ya kupuuza na kukiuka
sheria za usalama barabarani.

Aidha Jeshi la Polisi Dar es Salaam linatambua kuwa tarehe 31 Mach2025 au April 01 2025 kutakuwa na sikukuu ya Eld-el-fitri kutegemea kuandama kwa mwezi. Kutokana na
umuhimu wa sikukuu hiyo, suala la usalama limewekewa uzito mkubwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam zikiwemo fukwe za bahari ili sikukuu hiyo isherehekewe kwa amani.

“Niwasisitize wazazi na walezi kutowaacha watoto kwenda katika kumbi na maeneo mbalimbali bila kuwa na uangalizi kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea watoto kupotea, kupata ajali au kufanyiwa vitendo vinavyoweza kuhatarisha afya na maisha yao,” amewasihi Kamanda Muliro.

Jeshi la Polisi linawatakia kila la heri na linatoa wito kwa wananchi wote Dar es Salaam kusherehekea sikukuu ya Eid kwa amani na utulivu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here