Home UCHUMI TCB KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA UCHUMI IMARA

TCB KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA UCHUMI IMARA

Dar es Salaam

BENKI ya Biashara ya Tanzania ( TCB) imesema dhamira yake ni kushirikiana na Serikali katika kujenga uchumi imara na kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.

Akizungumza Machi 28, 2025 jijini Dar es Salaam wakati wa Iftari iliyoandaliwa na benki hiyo na kuwakutanisha wadau mbalimbali, Mkurugenzi Mkuu wa TCB Adam Mihayo amesema wameendelea kuwa wadau na kugusa sekta mbalimbali nchini.

“Tumeendelea kutoa misaada kwa kuimarisha miondombinu katika elimu ikiweo kusaidia madawati katika baadhi ya shule lakini pia tumetembelea katika hospitali na kutoa misaada bila kusahau makundi yenye uhitaji,” amesema Mihayo.

Amesema kwa kutambua unyeti wa baadhi ya sekta wamekuwa wakizigusa moja kwa moja ili kupunguza mzigo kwa serikali lakini pia ni sehemu ya kurudisha kwa jamii.

Ameongeza kuwa dhamira yao ni kuimarisha maendeleo jumuishi kwa jamii lakini pia kuendelea kutoa huduma bora kwa Watanzania huku akisisitiza matumizi ya huduma za kidigitali za benki hiyo.

Kwa upande wake Naibu Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Hassan Chizenga ambaye amemuwakilisha Mufti Mkuu wa Tanzania ameipongeza benki hiyo kwa kuandaa tukio hilo lililoweka pamoja watu tofauti katika jamiii akisema kuwa hio ndio maana halisi ya kujali.

Aidha ameitaka benki hiyo kuendelea kuigusa jamii ili kuonesha kwa vitendo ukongwe wa benki hiyo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali ikiwemo viongozi wa dini, watoto kutoka vituo vya kulea watoto yatima, wafanyakazi wa TCB, wateja wao pamoja na Jumuiya ya watu wenye ulemavu wa ngozi( Albinism).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here