Na Boniface Gideon, Tanga
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC)ambao pia ni wadhamini wa Ligi kuu na Ligi daraja la kwanza nchini,jana wamekabidhi Basi la kusafiria wachezaji pamoja na Benchi la ufundi ,basi hilo aina ya Yutong lenye uwezo wa kubeba abiria Kati ya 37-57 ,ni sehemu ya utaratibu wa Benki hiyo ,kuzikopesha club zinazoshiriki Ligi zinazoshaminiwa na Benki hiyo.

Akikabidhi Basi hilo Machi, 22 2025 kwenye Ofisi za Tawi la Benki hiyo jijini Tanga,Kaimu Mkurugenzi wa benk ya NBC Alvis Ndunguru , aliwaeleza wadau wa michezo kuwa,kutolewa kwa Basi hilo ni sehemu ya mikakati wa Benki hiyo katika kuboresha sekta ya michezo nchini hususani kwenye vilabu shiriki.
“Huu ni mkakati wetu wa kuboresha sekta ya michezo nchini na kuziwezesha timu za Ligi kuu na Ligi daraja la kwanza kuwa Mazingira Bora zaidi ,tulianza kwa timu 3 ambazo ni Namungo,Kmc ,Singida Black Stars na sasa ni Coastal Union,na kama Kuna timu nyengine inaweza ikaleta maombi ,milango ipo wazi kwa timu zote,” ameongeza Ndunguru.

Kwaupande wake,Mwenyekiti wa Coastal Union Muhsin Hassan,aliishukuru Benki hiyo kwakuwapatia Basi hilo la kisasa nakwamba hiyo ilikuwa ni kiu ya muda mrefu waliokuwa nayo mashabiki ,wapenzi na wanachama wa Coastal Union juu ya kumiliki usafiri wakisasa na sasa umepatikana.
“Tunashukuru sana ,Benki ya NBC kwa kutusaidia kupata usafiri, suala hili la usafiri lilikuwa ni tatizo kubwa sana kwetu japo kuwa tulishawahi kuwa na usafiri lakini ulikuwa haukidhi mahitaji yetu,”amesema Muhsin.