Home BIASHARA SERIKALI IMETANGAZA KUFANYA SENSA YA VIWANDA REJEA YA MWAKA 2023

SERIKALI IMETANGAZA KUFANYA SENSA YA VIWANDA REJEA YA MWAKA 2023

Dar es Salaam

SERIKALI imetangaza kufanya sensa ya uzalishaji wa viwanda rejea ya mwaka 2023 kubaini mchango wa viwanda katika ukuaji wa uchumi.

Kauli hiyo imetolewa leo Machi, 20 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk.Selemani Jafo alipokutana na wamiliki wa viwanda katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

“Takwimu za sensa hii zinamaana kubwa kwa taifa kwani zitaonesha nchi inasongaje mbele kimaendeleo na tena zitaisaidia serikali kupanga mipango yake,” amesema.

Amesema sensa wanayotarajia kuifanya ina lengo la kuona nchi kmefikia wapi katika mipango ya maendeleo na kuona jinsi viwanda vinavyotoa mchango kwa ukuaji wa uchumi.

Dk.Jafo amesema sensa hiyo itafanyika Tanzania Bara na Zanzibar na anaamini itafanyika kwa ufanisi kwa sababu uzalishaji viwanda ni muhimu kwa mstakabadhi wa maendeleo ya viwanda.

“Nchi mbalimbali duniani zinazojinasibu kwa maendeleo lazima wawe na takwimu hivyo tutahakikisha tunapata takwimu sahihi zitakazosaidia upatikanaji wa sera na mipango mikakati mbalimbali ya kimaendeleo.

“Hivyo serikali ipo tayari kusikiliza hoja na changamoto mbalimbali katika viwanda kusaidia uwekezaji kusonga mbele,”amesema.

Naye Kamisaa ya Sensa ya Watu na Makazi, Anne Makinda aliomba ushikiriano kwa wenye viwanda kupata taarifa sahihi kutengeneza sera na sheria zinazostahili.

“Bila sensa hatuwezi kufanya chochote kwa mafanikio hivyo wafanya sensa watunze siri na wenye viwanda watoe ushirikiano kuwezesha utungaji wa sera nzuri,”amesema.

Kwa upande wake, Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk. Amina Msengwa amesema sensa hiyo itachangia kutekeleza ukuaji uchumi wa viwanda nchini kwani takwimu ni nyenzo ya kufanya maamuzi kufanya maamuzi yenye ufanisi.

Amesema sensa hiyo itatoa viashiria muhimu kulingana na wakati na itahusisha kupata taarifa ya kiwanda, ajira ya viwandanu na muda wa kazi.

Pia itahusisha gharama za ajira, gharama za uzalishaji, bidhaa zilizozalishwa na mauzo, thamani ya mali zilizopo gharani na nyinginezo hivyo itafiti huo utasaidia kupata taarifa za awali zitakazosaidia kujipima kwa miaka 25 iliyopita.

Naye, Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini (CTI), Husein Sufuan amesema viwanda watahakikisha wanaendeleza ushirikiano katika utendaji wa kazi na takwimu hizo zitatoa picha halisi za viwanda nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here