Dar es Salaam
MSANII nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa, Rayvanny, maarufu kama Chui, ameizindua rasmi promosheni mpya inayojulikana kama “Kula Shavu”, kwa kushirikiana na kampuni ya mchezo wa kubashiri Pigabet.

Akizungumza leo Machi 19, 2025, jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo, Rayvanny amesema kuwa wateja wapya watakaojisajili kwa kutumia kodi ya “CHUO” watajipatia bashiri za bure zenye thamani ya shilingi 30,000.
Kwa mujibu wa Rayvanny, wateja wote wa “Kizazi cha Wajanja” wa Pigabet wanapaswa kubashiri kwa dau la kuanzia shilingi 2,000 na kuendelea, huku mkeka ukiwa na mechi mbili au zaidi ili kushiriki katika promosheni hiyo.

Kwa upande wake, Afisa Habari wa Pigabet, Allen Mwinyi, amesema kuwa promosheni hiyo itatoa nafasi kwa washindi 10 kutangazwa kila wiki, ambapo kila mmoja atajishindia shilingi 500,000.
“Zaidi ya hayo, washindi watano wa mwisho wa mwezi kila mmoja atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 2. Kwa ujumla, ndani ya mwezi mmoja, tutakuwa na zaidi ya washindi 300,” alisema Mwinyi.
Promosheni ya “Kula Shavu” imeanza rasmi leo Machi 19, 2025, na itaendelea hadi Aprili 20, 2025. Mwinyi amesisitiza kuwa mwaka huu, Pigabet imejipanga kutoa burudani zaidi, zawadi kubwa, na huduma bora kwa wateja wao wa kubashiri.