Home KITAIFA RAIS DK. SAMIA : HAKIKISHENI KUNAKUWA NA UDHIBITI ENDELEVU WA UPOTEVU MAJI

RAIS DK. SAMIA : HAKIKISHENI KUNAKUWA NA UDHIBITI ENDELEVU WA UPOTEVU MAJI

Kilimanjaro

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Maji na watu walioaminiwa kuhakikisha kuwa huduma ya maji kwenye Wilaya za Same, Mwanga Mkoani Kilimanjaro na Korogwe Mkoani Tanga zinakuwa endelevu sambamba na kuwa na udhibiti endelevu wa upotevu maji.

Hayo ameyasema leo Machi, 9 2025 mkoani Kilimanjaro Rais Dk.Samia wakati akizindua mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe ameelekeza Waziri Aweso kuhakikisha kuwa vijiji 10 vinazunguka Bwawa la Nyumba ya Mungu vinakuwa na huduma ya maji.

“Vijijini hivi ni muhimu kuwa na ulinzi wa miundombinu na vyanzo vya maji wilayani hii lakini la tatu ni ulinzi wa miundombinu na vyanzo vya maji mradi huu ni mkubwa mno ukienda ukaharibika tumeharibikiwa na eneo kubwa watu laki tatu wameharibikiwa na tumeharibikiwa kupata maji,” Rais Dk.Samia.

Amesisitiza umuhimu wa Wakuu wa Mkoa na Wilaya kusimamia ulinzi wa vyanzo vya maji na miundombinu ya mradi huo na umuhimu wa waziri kutoruhusu ulimbikaji wa bili za maji kwa kutafuta mita zitakazowaruhusu wananchi kulipa kabla ya matumizi.

Rais Dk.Samia amesema kukamilika kwa mradi huo kunatarajia kuwa na mchango katika kupunguza umaskini kwa jamii kutoa muda zaidi kwa wananchi kujishughulisha na uzalishaji wa mali badala ya kutumia muda mrefu kutumia huduma ya maji.

“Kukamilika kwa mradi huu utakao hudumia wananchi zaidi ya 300000 na kusaidia katika kuimarisha afya za wananchi wa mikoa ya Kilimanjaro na Tanga kwani kutawaepusha wananchi na magonjwa mbalimbali ambayo yanatokana na matumizi ya maji yasiyokuwa safi na salama,”ameeleza.

Amesema mradi huo unatarajia kuvutia wa wekezaji katika wilaya hizo hasa kwa wawekezaji ambao ni wazalishaji wa bidhaa zao umekuwa ukitegemea huduma ya maji.

Rais Dk.Samia mradi huo utatoa fursa kwa wasichana kupata mda mrefu zaidi kujisomea na kutotumia muda mrefu kutafuta huduma ya maji kama itakavyorahisisha pia shughuli kwa wanawake.

“Kukamilika kwa mradi huu kunawezesha upatikanaji wa maji ya uhakika wa lita milioni 6 kutoka za awali za lita milioni 3.7 kwa siku ukitarajia kuhudumia wananchi takribani 300000 kutoka 50 615 wa awali sambamba na kutoa huduma ya maji bila mgao tofauti na awali,”amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here