Na Esther Mnyika, Mtwara
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema Mpango wa Ununuzi wa Dhahabu nchini haina nia ya kuvuruga soko la dhahabu nchini hivyo imefanikiwa kununua zaidi ya tani mbili ya dhahabu ndani ya miezi mitano huku lengo kufikia tani sita kwa mwaka.

Hayo aliyabainisha Februari, 25 2025 Mkoani Mtwara Mchambuzi wa Masoko ya Fedha kutoka BoT, Dunga Nginila wakati akiwasilisha mada ya umuhimu wa Akiba ya Dhahabu kama Sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Fedha za Kigeni katika mafunzo ya waandishi wa habari wa habari za uchumi, biashara na fedha katika mikoa ya Dar es Salaam, Ruvuma, Lindi, Mtwara na visiwa vya Zanzibar.
Amesema lengo la kufanya hivyo ni kuongeza akiba ya dhahabu, kuongeza akiba ya fedha zakigeni na kuinua soko la madini nchini.
“Hadi sasa tuna akiba ya dhahabu fedha zaidi ya tani mbili huku lengo likiwa kufikia tani sita kwa mwaka na tumeanza kununua dhahabu kutoka Tanzania tangu Oktoba mwaka jana ambapo lengo ni kufikisha tani sita kabla ya mwaka wa fedha kuisha,”amesema.
Ameeleza kuwa dhahabu ina faida kubwa kweye nchi kama yetu ambayo wana dhahabu nyingi. kwahiyo faida kubwa ni kuongeza akiba fedha za kigeni za nchi. na dhahabu fedha wqnapoinunua na kuifikisha kwa wateja wao inakuwa inahesabika kama fedha za kigeni za nchi na waumekuwa wakinunua dhahabu kila siku na wananunua kutoka Tanzania tu kwani bado kuna akiba nyingi ya dhahabu.

“Dhahabu ina faida kubwa, hususani nchi kama yetu ambayo tumejaliwa kuwa na dhahabu nyingi, kwa kikubwa ni kwamba tunaongeza akiba ya fedha za kigeni za nchi hususani dhahabu fedha, tunapoinunua tunapoifikisha katika ulinzi wetu inahesabika kama fedha za kigeni za nchi.
“Kwa hiyo mpaka sasa tume-‘accumulate’ tani zaidi ya mpaka sasa, huku lengo la Benki Kuu ni kununua sita kwa mwaka, na tunatarajia kufikiria mbili hilo lengo kabla ya mwaka wa fedha huu kukamilika, kitu cha muhimu na msingi ni tunanunua dhahabu ya Tanzania tu, si dhahabu ya nchi nyingine mpango wa BoT, tunanunua dhahabu kila siku kwa sababu tuna malengo ya mwaka ya tani sita,” amesema.
Amesema mpango wa ununuzi wa dhahabu umekuwa ukitoa fursa kwa wauzaji wa dhahabu nchini kuuza dhahabu zao moja kwa moja BoT kwa bei yaushindani wa Soko la Kimataifa.
Ameongeza kuwa mpango wa ununuzi wa dhahabu ulianza Oktoba, mwaka jana kwa kuwawezesha wazuzaji dhahabu kupata punguzo ada na uhakika wa malipo ya haraka na wakiuza kwa asilimia 20 ya dhahabu na bei inayotumika ni ile ya dhahabu duniani kama inavyotolewa na Tume ya Madini ambapo huwa inabadilika kila siku.
Nginila amesema wamekuwa wakinunua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wakubwa na wadogo kwa lengo la kuongeza akiba akiba kutofautisha akiba za fedha na kukuza sekta ya uchimbaji madini ya ndani ya nchi.