Na Deborah Lemmubi-Dodoma.
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dk. Erasmus Kipesha amesema kuwa Mamlaka hiyo itaendelea kuzingatia ushauri wakati wote wanapotekeleza majukumu yao ili kufanikisha azma ya Serikali ya awamu ya sita inayolenga kila mtoto wa Kitanzania kupata fursa ya elimu bora.

Dk. Kipesha amesema hayo Leo, Februari, 25 2025Jijini Dodoma Februari 25,2025 wakati akizungumza na waandishi wa Habari akielezea mafanikio ya Mamlaka hiyo kuelekea Maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.
Ameishukuru Serikali hiyo inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga fedha kwaajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo chini ya Mfuko wa Elimu unaoratibiwa na TEA.
“Mamlaka itaendelea kuzingatia ushauri katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila mwaka kwaajili ya kufanikisha azma ya Serikali ya awamu ya sita inayolenga kuhakikisha kuwa kila mtoto wa Kitanzania anapata fursa ya elimu bora,”.
Aidha Dk. Kipesha amesema kuwa watahakikisha wanaimarisha miundombinu ya elimu kote nchini kwa kuunga mkono jitihada na utekelezaji wa Sera kwa kuwa na miundombinu bora na vifaa vya amali.

“Jukumu letu kubwa ni kuimarisha na kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia kwa kujenga vyumba vya madarasa,matundu ya vyoo,nyumba za walimu,maabara,mabweni pamoja na kuweka vifaa mbalimbali vya elimu vya mafunzo ya amali,”amesema.
Kwa upande wa utekelezaji wa Sera mpya ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023, amesema Mamlaka hiyo imetenga Shilingi Bilioni 3 kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu na vifaa mbalimbali vya mafunzo amali kwa shule 20 nchini.
Amesema ni wajibu wao ni kuhakikisha wanaunga mkono utekelezaji wa sera hiyo ya elimu kwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa maana ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, maabara za Sayansi,nyumba za walimu na vifaa mbalimbali vya mafunzo ya amali kama michezo,ushoni, mapishi,kilimo,Sanaa na Tehama.
Amesema Rais Dk.Samia kuwakomboa vijana wa Kitanzania kwa kuboresha Sera ya Elimu na Mafunzo ambapo vijana wataweza kujiajiri kutokana na ujuzi watakaoupata wawapo mashuleni.
Pia ametoa wito kwa wadau wa elimu nchini kuendelea kuiunga mkono Serikali kwa kuchangia Sekta ya elimu kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa.
TEA ni moja ya Taasisi za Serikali zinazowalisha mafanikio waliyoyapata ndani ya miaka minne ya Uongozi wa Dk. Samia.