Home KITAIFA MUHONGO :UVUVI WA VIZIMBA UNATAINUA UCHUMI MKUBWA WA WANANCHI MUSOMA VIJIJINI

MUHONGO :UVUVI WA VIZIMBA UNATAINUA UCHUMI MKUBWA WA WANANCHI MUSOMA VIJIJINI

Na Shomari Binda-Musoma

UVUVI wa samaki kupitia njia ya vizimba umedaiwa kuwa moja ya njia ya kuinua uchumi mkubwa wa wananchi wa jimbo la Musoma vijijini.

Hayo yamesemwa leo Februari, 17 2025 na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo baada ya kuelezwa na wavuvi hao namna wanavyonufaika na uvuvi huo.

Muhongo amesema wavuvi kwa kuendelea kuzingatia maelekezo ya wataalam na maafisa uvuvi wanakwenda kuondokana na umasikini.

Amesema ziwa Victoria lina umri wa takribani miaka 400,000 na ujazo wake wa kawaida ni kilomita za ujazo 2,760 (2,760 cubic kilometres).

Ameeleza kuwa mvua za mwaka jana ziliongeza ujazo wa maji ndani ya bonde la Ziwa Victoria lenye ukubwa kilomita za mraba 195,000 (195,000 square kilometres)lilikuwa na ongezeko la kina cha takribani mita 1.7 (ca. 1.7 meters depth)

Mbunge huyo amesema Kata 18 kati ya Kata 21 za jimbo zina ufukwe wa Ziwa Victoria kwa hiyo asilimia 85.7 (85.7%) za Kata zina fursa nzuri za kutumia raslimali za maji ya Ziwa hilo.

“Samaki wamepungua sana ndani ya Ziwa Victoria na mito inayolizunguka. Suluhisho la tatizo hili ni kuanzisha na kuendeleza uvuvi wa ufugaji wa samaki ziwani humo (aquaculture fish farming)

“Upungufu wa samaki haupo tu ndani ya Ziwa Victoria bali ni tatizo kubwa ulimwenguni kote Bahari, maziwa na mito ya duniani kote ina upungufu mkubwa wa samaki”,amesema.

Muhongo amesema kwa sasa takribani nusu (ca. 50%) ya samaki duniani kote wanapatikana kupitia ufugaji wa samaki ndani ya bahari, maziwa kupitia (aquaculture fish farming).

Amesema mitaji ya uvuvi wa vizimba kutoka mikopo nafuu ya serikali Kuu vizimba 8 tayari vimetayarishwa na kuwekwa ziwani na uzalishaji utaanza ndani ya miezi 3 ijayo na mikopo kutoka kwenye ma benki huku vizimba 10 vya watu binafsi vikiendelea na shughuli.

Baadhi ya wavuvi wa vizimba wa Musoma Vijijini wamemueleza mbunge huyowa kwamba kwenye kizimba kimoja chenye kipenyo cha mita 10 (10m-diameter) wamefanikiwa kuvuna tani 12 za samaki wenye thamani ya Tsh milioni 100 (Tsh 100m).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here