📌 Awaalika wadau EAC kushiriki Kongamano la 11 la Afrika Mashariki la Mafuta na gesi
📌 Asema Tanzania inazo rasilimali za kutosha kwenye mafuta na gesi
📌 Kongamano kufunguliwa rasmi na Dkt Samia Suluhu Hassan
Dar es salaam
KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, amewataka Watanzania kutumia fursa za kongamano la 11 na maonesho ya Afrika Mashariki ya mafuta na gesi kunadi fursa za uwekezaji hapa nchini ili kuvutia wawekezaji.
![](https://www.lajiji.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/1001195449-1024x683.jpg)
Mhandisi Mramba ameyasema hayo leo 6 Februari, 2025 jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya kongamaano la EAPC’E ambapo Tanzania ndio mwenyeji wa kongamano hilo kwa mwaka huu na linabeba kauli mbiu ‘’ kufungua fursa za uwekezaji katika Nishati: Mchango wa rasilimali za mafuta katika kupata Nishati ya uhakika kwa maendeleo endelevu ya Afrika Mashariki’’
Amesema kwa sasa Tanzania inahitaji vyanzo mbalimbali vya nishati safi ili kuepuka athari za mazingira hivyo ujio wa mkutano wa EAPC’E25 unafanyika kwa muda sahihi ambapo Afrika imeweka lengo la kufikisha umeme kwa waafrika milioni 300 kufikia mwaka 2030 na ndio maana nchi za Afrika Mashariki zinachukua hatua ya kujadili umuhimu wa rasilimali za mafuta na gesi kufikia malengo hayo.
![](https://www.lajiji.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/1001195509-1024x683.jpg)
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya EAPCE’25 ambaye pia ni Naibu katibu Mkuu anayeshughulikia Mafuta na Gesi Dk. Jamea Mataragio amesema mkutano huo una umuhimu wa kipekee kwakuwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki zitakuwa na uwezo wa kubadilishana utaalamu na uzoefu kwenye sekta ya mafuta na gesi pamoja na kijadili changamoto zilizopo na namna ya kukabiliana nazo.
![](https://www.lajiji.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/1001195521-1024x683.jpg)
Amesema washiriki zaidi ya 1,000 wanatarajia kushiriki mkutano huo kutoka nchi nane za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, Kenya, uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan kusini.