Home KITAIFA SERIKALI KUPITIA UPYA MASILAHI YA WALIMU.

SERIKALI KUPITIA UPYA MASILAHI YA WALIMU.

Dodoma

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan Ameitaka Wizara ya Fedha, Wizara ya Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI kuwezesha na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Sera na mitaala mipya ya elimu ili ilete matokeo yaliyokusudiwa katika kuimarisha sekta ya elimu.

Pia amesema Serikali itapitia upya masilahi ya Walimu ili kuipa hadhi kada hiyo.

Kauli hiyo ametoa Februari 1, 2025 Jijini Dodoma Rais Dk. Samia wakati akizindua sera ya hiyo iliyokwenda sambamba na kaluli mbiu isemayo “Elimu na ujuzi ndio mpango mzima”.

Amesema mabadiliko na kukua kwa kasi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA ) kunaweza kuwa na mchango chanya au hasi kutokana namna jamii itakavyojipanga.

“Ili kuendelea na mabadiliko haya ni lazima kutumia TEHAMA kutoa elimu kwa urahisi na kuandaa vijana wetu kuwa na taaluma za ujuzi wa taaluma zinazoendana na mageuzi ya TEHAMA bila kuathiri kuathiri maadili ya vijana hawa,”amesema.

Amesema serikali haina budi kuwa na maandalizi ya kutosha kwa kuinua viwango vya ubora wa elimu, na kuwaanda vijana vizuri zaidi ili waweze kumu du stadi muhimu zitakazowawezesha kuajiriwa na kujiajiri pamoja na kuwajengea ujasiri na kuweza kujiamini.

Rais Dk.Samia amesema dhamira ya kufanya mabadiliko katika sera ni kumuaandaa kijana anayejiamini na mwenye nyenzo stahiki za kukabiliana na ushindani wa kikanda na kimataifa ili kutumia utajiri wa rasilimali zetu aweze kunufaika kiuchumi.

Amesema ili kuwa na elimu Bora na utekelezaji wa mitaala iliyoboreshwa ni lazima kuboresha maslahi ya walimu ambayo ni mama wa elimu zote Duniani na huku akisisitiza Walimu kuendelea kupewa mafunzo mbalimbali

Aidha, Dk. Samia ameiagiza Ofisi ya Rais -TAMISEMI kuandaa mkakati maalum wa kuteleza sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014, toleo la 2023 katika upande wa mioundombini.

Naye Rais Mstaafu wa wamu wa Nne na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (GPE), Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa wadau wa maendeleo wanafuatilia kwa hatua kubwa mendeleo ya sekta ya elimu nchini na wanalidhishwa nayo huku akiweka bayana mapendekezo yao.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Muhamed Mussa amekiri kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mchakato huo wa sera wameshirikiana katika kila hatua ili waweze kufanikisha mchakato huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here