Dar es Salaam
TIMU ya Simba SC ya Tanzania imeonyesha ubora wa soka dhidi ya Timu ya CS Constantine_officiel kutoka Tunisia mara baada ya kuifunga jumla ya mabao mawili kwa sifuri (2-0) katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika ambao umechezwa leo Januari, 19 2025 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kutafuta Kinara wa Kundi A kufuatia timu hizo kuwa tayari zimeshafuzu hatua ya Robo fainali ya michuano hiyo Simba SC ndio iliyojihakikishia kuongoza kundi hilo baada ya kupachika magoli mawili yaliyofungwa na Mchezaji wao Machachari Kibu Dennis na Lionel Ateba.
Hata hivyo ushindi huo wa Simba unaifanya kufikisha alama 13 kwenye msimamo wa Kundi A huku CS Constantine wakishika nafasi ya pili kwa alama 12 ,Bravos ya Angola nafasi ya tatu na CS Sfaxien wakaburuza mkia nafasi ya nn