Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Hussein Ali Mwinyi ameizawadia Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes shilingi milioni 50 baada ya kulitwaa Kombe la Mapinduzi 2025.
Akizungumzaleo Januari, 15 2025 katika hafla maalum ya chakula cha mchana aliyoiandaa kwa ajili ya wachezaji wa timu hiyo katika Viwanja Vya Ikulu, Rais Dk. Mwinyi ameeeleza kuwa timu hiyo imeiletea Heshima kubwa Zanzibar na kudhihirisha kuwa kuna vipaji vingi vya Soka hapa nchini vinavopaswa Kuendelezwa katika Maeneo mbalimbali.
Amefafanua kuwa kwa mafanikio ya Zanzibar Heroes kuna kila sababu kwa Serikali kuendelea na Ujenzi wa Academy za Soka Kila Mkoa kwa Lengo la Kuviibua vipaji vya vijana.
Rais Dk. Mwinyi ametangaza dhamira ya kuunda kamati maalum ya Kitaifa hivi karibuni itakayokuwa na jukumu la kumshauri namna bora ya kuuendeleza mpira wa miguu hapa nchini.
Ameeleza kuwa hatua za timu za Zanzibar Kulibakisha Kombe la Mapinduzi kwa Mwaka wa tatu mfululizo kunaashiria uwezo mkubwa wa soka na vipaji viliopo .
“Wengi tulishtuka tuliposikia timu za Afrika Magharibi zinakuja kushiriki Mmchuano ya mapinduzi,Lakini mumefanya kazi nzuri asanteni sana,” amesema Dk. Mwinyi.
Amefafanua kuwa tayari wataalamu wa soka (SCOUT) wa Nchini Uturuki wameonesha nia ya kuja Zanzibar baada ya kuushuhudia mchezo wa fainali baina ya Zanzibar na Burkinafaso na kukiri kuwepo vipaji vingi.
Dk. Mwinyi amesisitiza kuwa lengo ni kuwa na timu Imara za mpira wa Miguu katika ngazi zote zitakazoiletea heshima Zanzibar.
Rais wa Shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFF), Suleiman Mahmoud Jabir ametumia fursa hiyo Kumkabidhi Rais Dk.Mwinyi Kombe la Mapinduzi 2025.