Home KITAIFA RAIS DK.MWINYI: WAZAZI NA WALIMU WANA JUKUMU MUHIMU LA KUWASIMAMIA WATOTO KUSOMA...

RAIS DK.MWINYI: WAZAZI NA WALIMU WANA JUKUMU MUHIMU LA KUWASIMAMIA WATOTO KUSOMA KWA BIDII

Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema wazazi na walimu wana jukumu muhimu la kuwasimamia watoto kusoma kwa bidii baada ya Serikali kuandaa mazingira mazuri ya kusomea.

Rais Dk,Mwinyi ametoa tamko hilo leo Januari, 9 2025 alipoifungua Skuli Mpya Ya Msingi ya Kojani , Wilaya Ndogo ya Kojani,Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Dk.Mwinyi ameeleza kuwa ujenzi wa skuli unaofanywa na serikali lengo lake ni kuhakikisha watoto wanapata fursa nzuri ya elimu katika mazingira bora.

Akizungumzia Skuli Ya Kojani Rais Dk.Mwinyi ameeleza kufarijika na kazi nzuri ya usimamizi uliofanywa na watendaji wa wizara ya elimu na mafunzo ya amali na Wakala wa Majengo pamoja na Mkandarasi kwa Kumaliza Ujenzi huo kwa wakati na kwa viwango bora.

Akizungumzia suala la ajira ameziagiza Wizara ya Afya ,Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na Utumishi kuhakikisha ajira zinapofanyika hususan kojani ni lazima wapewe vijana wa kisiwa hicho na Kuzitaka taasisi hizo kusimamia agizo hilo.

Agizo jengine amelitoa kwa Wizara ya Afya kuipeleka boti moja ya Matibabu Kojani Miongoni mwa boti tano zilizoagizwa na wizara hiyo.

Amefahamisha kuwa hatua hiyo itaongeza Wepesi wa utoaji wa huduma kwa wananchi wa kojani.

Aidha Rais Dk. Mwinyi amesisitiza kuwa Serikali Itaongeza Wafanyakazi Kojani ili huduma ndogondogo katika nyanja mbalimbali zitolewe Kisiwani .

Akizungumzia Michezo amewahakikishia wananchi kuwa Serikali Inakusudia kutoa Upendeleo maalum kwa Ujenzi wa Kiwanja cha Kisasa cha Michezo pamoja na Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Kisiwani humo.

Akizungumzia Mabadiliko ya Tabia nchi na tatizo la maji ya bahari kuingia Katika makaazi ya watu Dk.Mwinyi ameahidi kwa serikali kukaa na wataalamu kulipatia ufumbuzi suala hilo.

Akitoa taarifa ya kitaalamu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Khamis Abdalla Said amesema Ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Kojani Umegharimu shilingi bilioni 5.382 ikiwa na Madarasa 32,Maabara ,Chumba cha Kompyuta, Maktaba na Ukumbi wa kufanyia Mitihani ina Uwezo wa kuchukua Wanafunzi 1,305 kwa Mkondo Mmoja
Mke wa Rais.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here