Zanzibar
MKE wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi ametoa Rai kwa Wadau Zaidi kuunga Mkono Juhudi za Kumaliza Changamoto wanazokabiliana nazo watoto wa Kike wanapokuwa Skuli.
Mama Mariam ambae Pia ni Msarifu wa Zanzibar Maisha Bora Foundation ametoa rai hiyo leo Januari,9 2025 katika ufunguzi wa Skuli Mpya ya Msingi Kojani ,Wilaya Ndogo Kojani, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Amefafanua kuwa qanafunzi wengi wa kike wamekuwa wakikabiliana na changomoto nyingi zinazodhorotesha kiwango chao cha elimu ,Utoro na kukatisha masomo hususani wanapokuwa katika ada zao za mwezi.
Amesema wakati umefika kwa wadau kuunganisha nguvu za pamoja kuwasaidia wanafunzi wa kike kutimiza ndoto zao za kielimu.
Mama Mariam ameeleza kuwa taasis hiyo tangu Mwaka 2022 imekuwa na utaratibu wa kugawa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike na tayari imewafikia wanafunzi 5,676 Unguja na Pemba.
Aidha amesisitiza kuwa taasisi jiyo imeandaa programu mpya yenye lengo la kuwapatia wanafunzi wa kike 3000 taulo za kike na tayari imewafikia wanafunzi 643 wa Wilaya ya Kusini na kati Unguja.
Aidha Mama Mariam Mwinyi amesema taasisi hiyo imepanga tumaini Kit 777 ,soksi na viatu 5,548
watapatiwa wanafunzi wa kike wa skuli za msingi na sekondari.
Mke wa Rais Wa Zanzibar ameishukuru Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na Taasisi ya Infinity Foundation kwa kuwa wadau muhimu kwa Maendeleo ya Taasisi hiyo na juhudi za kuwakomboa watoto wa kike nchini.
Hafla hiyo ya ufunguzi wa Skuli ya Kojani iliambatana na ugawaji wa taulo za Kike kwa wanafunzi wa kike wa Kojani.
Ufunguzi huo wa Skuli ya Msingi Kojani ni miongoni mwa Shamrashamra za Sherehe za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.