Home KITAIFA RAIS DK.MWINYI:WANANCHI WANAOISHI PEMBEZONI MWA BARABARA KUFUATA SHERIA

RAIS DK.MWINYI:WANANCHI WANAOISHI PEMBEZONI MWA BARABARA KUFUATA SHERIA

Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza Wananchi wanaoishi Pembezoni mwa Barabara ya Kizimbani – Kiboje kufuata Sheria na kutojenga katika Eneo la Hifadhi ya Barabara hiyo.

Rais Dk, Mwinyi ametoa tamko hilo leo Januari, 02 2025 wakati akiweka jiwe la Msingi la Barabara ya Kizimbani -Kiboje Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja yenye Urefu wa Kilomita 7.225 iliojengwa kwa Kiwango cha lamI

Amefafanua kuwa ni vema kwa Wananchi kutojenga katika eneo la Hifadhi ya Barabara ili libaki kwa Shughuli nyengine za kijamii ikiwemo kupitisha Miundombinu mengine ikiwemo Maji, Umeme na Mawasiliano .

” Kazi Nzuri iliofanywa na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mshauri Elekezi na Kampuni ya CCECC kwa kusimamia Ujenzi huo aliouelezea kuwa na Ubora na viwango stahiki vya barabara za kisasa,”amesema.

Rais Dk,Mwinyi ameeleza kuwa Sekta ya Ujenzii ni Miongoni mwa Sekta iliofanya vizuri katika Utekelezaji wa Majukumu yake kwa Kazi nzuri ya Ujenzi wa Madaraja, Barabara katika maeneo mbalimbali ya Nchi.

Rais Dk, Mwinyi amewanasihi Wananchi Kuendelea kuishi Kwa Amani na Umoja ili Nchi iendelee kutekeleza Miradi ya Maendeleo zaidi.

Naye Waziri wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk, Khalid Muhammed Salum amesema Ujenzi wa Barabara hiyo ni kichocheo cha Ukuaji wa Uchumi kwani imejengwa katika Maeneo muhimu ya Kilimo yenye rutuba inayozalisha Mazao mengi.

Ameelezea Ujenzi huo.kuwa ni wa Upendeleo maalum kwa Wananchi wa Kizimbani,Mndo na Kiboje baada ya kusubiri kwa takriban miaka 40 bila ya kuwa na Barabara ya kiwango cha lami.

Akiwasilisha Taarifa ya Kitaalamu ya Ujenzi wa Barabara hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk, Habiba Hassan ameeleza kuwa Ujenzi wa Barabara hiyo ya Kizimbani -Kiboje yenye Urefu wa Kilomita 7.225 ni Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025 ,Dira ya Maendeleo ,Mpango wa Maendeleo wa Taifa , Sera ya Taifa ya Usafiri na Mpango Mkuu wa Usafiri.

Aidha amefafanua kuwa Ujenzi huo umefikia asilimia 85 na utakapokamilika utagharimu Dola za Marekani Millioni 6.265 na itakuwa na Uwezo wa kutumika kwa Miaka 25 ijayo.

Ujenzi wa Barabara hiyo Unaendelea chini ya Kampuni ya CCECC unatarajiwa kukamilika Mwezi Mei Mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here