Home KITAIFA DK.MWINYI: VIONGOZI NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KUENDELEA KUIOMBEA NCHI AMANI

DK.MWINYI: VIONGOZI NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KUENDELEA KUIOMBEA NCHI AMANI

Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Viongozi na Waumini wa dini ya Kiislamu kuendelea kuiombea nchi
Amani wakati huu ikielekea kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Alhaj Dk, Mwinyi ametoa tamko hilo Disemba, 29 2024 alipotoa salamu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Madrassa Maryam ya Mfenesini Wilaya ya Kaskazini B, alipojumuika katika dua Maalum ya Kumuombea ilioandaliwa na Madrassa hiyo.

Ameeleza kuwa mambo yote ya Maendeleo yataweza kufanyika ikiwa nchi itabaki na Amani na Wananchi kuwa na Umoja na Utulivu wa nchi.

Amefahamisha kuwa hakuna nchi yenye machafuko iliopata Maendeleo hivyo kila mmoja ana wajibu wa kusisitiza Amani kwa maslahi ya nchi.

Alhaj ,Dk, Mwinyi ameeleza kuwa Uzoefu unaonesha kuwa kwa muda mrefu nchi ilikuwa ikipata matatizo hususan wakati wa Uchaguzi hivyo ni vema mambo hayo yasijirudie tena kwa kuhubiri Amani ndani ya Jamii.

Katibu Mtendaji wa Afisi ya Muft Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Mfaume amesema kabla ya mambo yote nchi ni lazima iwe na amani na watu wake wana wajibu wa kuiombea amani kwani ndio nyenzo muhimu kwa nchi inayohitaji Maendeleo.

Akisoma Risala ya Waumini wa Madrassa hiyo Sheikh Suleiman Muhammed Othman amesema jambo la kuombea dua hususan kwa Viongozi ni katika Ibada tukufu zilizotiliwa mkazo katika Dini ya Kiislamu.

Mlezi wa Madrssa hiyo Said Nasser Bopar ameahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za kuiendeleza Madrassa hiyo pamoja na kumuunga Mkono Rais Dk ,Mwinyi katika kuleta Maendeleo ya nchi.

Kabla ya Dua hiyo maalum Alhaj Dk, Mwinyi alimjulia hali Mwanzilishi wa Madrassa hiyo Maryam Omar Muhammed .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here