Home BURUDANI DISEMBA 26,2024 HISTORIA YA MASUMBWI NGUMI ZA KULIPWA KUANDIKWA TANZANIA

DISEMBA 26,2024 HISTORIA YA MASUMBWI NGUMI ZA KULIPWA KUANDIKWA TANZANIA

Dar es salaam

WASANII Filamu Nchini Bongo movie wametoa mitazamo yao kuelekea siku ya Disemba, 26 Masaki Jijini Dar es salaam siku ya boxing day maarufu siku ya kutoa zawadi kutakuwa na mapambano ya ngumi ya aina yake ambayo haijawahi kutokea Tanzania.

Usiku huo uliopewa jina la “Knockout ya mama” unatarajiwa kufanyika huku kukitegemewa kushuhudiwa mfululizo wa mapambano ya ngumi ya kimataifa ambapo mikanda mitano ya kimataifa ya ngumi itashindaniwa.

Akizungumza na wanahabari leo Desemba 18,2024 Jijini Dar es salaam msanii Jimmy Mafufu amesema amefurahishwa kampuni ya uandaaji mapambano ya ngumi ya Mafia boxing promotion kwa kuandaa tukio hilo kubwa kitaifa huku ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kuunga mkono jitihada za serikali katika kuinua michezo nchini.

Aidha mbali na msanii huyo wasanii wengine wa filamu akiwemo Wema Sepetu, Shamsa ford, Sakina Lyoka na wengine wametoa rai kwa wapenzi wa sanaa na wanamichezo kuungana kwa pamoja katika kushuhudia historia inayokwenda kuandikwa ambayo itakwenda kubaki kuweka alama ya mchezo huo kwa muda usiotabirika.

Usiku huo utahusisha jumla ya mabondia 13 wa kitanzania ambao watashuka ulingoni kupigana dhidi ya mabondia kutoka nchi mbalimbali ndani na nnje ya Afrika.

Usiku wa Knockout ya mama unatarajiwa kufanyika Disemba 26 katika ukumbi wa The super dome, masaki, Dar es salaam.

Aidha kutokana na wingi wa mabondia hivyo Desemba 20 mwaka huu kutakiwa na shindano litakalooneshwa bure makao makuu ya Boxing Magomeni wadau wote wanakaribishwa kujipatia burudani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here