Home KIMATAIFA DK. NCHEMBA AHITIMISHA ZIARA NCHINI OMAN

DK. NCHEMBA AHITIMISHA ZIARA NCHINI OMAN

Na Saidina Msangi, Muscat, Oman

WAZIRI wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Oman ambapo akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muscat – Oman, akielekea nchini Saudi Arabia ambako atakuwa na ziara nyingine ya kikazi, aliagwa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Fatma Rajab.

Akiwa nchini Oman, pamoja na mambo mengine, Dk. Nchemba alitia saini Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi ya Mapato Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji Kodi, ujulikanao kama An Agreement for the Elimination of Double Taxation with Respect to Taxes on Income and Prevention of Tax Avoidance and Evasion, wenye lengo la kukuza biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.

Aidha, Dk. Nchemba, amewasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kushiriki katika Jukwaa la Biashara na Uwekezaji, linalotarajiwa kufanyika katika Makao Makuu ya Chemba ya Biashara Riyadh, Saudi Arabia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here