Home KITAIFA WAZIRI ULEGA:HATOKUWA NA SUBIRA WALA UVUMILIVU KWA MKANDARASI MZEMBE

WAZIRI ULEGA:HATOKUWA NA SUBIRA WALA UVUMILIVU KWA MKANDARASI MZEMBE

Dar es Salaam

WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega amewaagiza wakandarasi wanaojenga Mradi wa Barabara ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) hatokuwa na subira wala uvumilivu kwa mkandarasi mzembe na anayefanya vizuri kazi yake atapongezwa na kupewa tenda nyingine.

Pia ametoa siku tatu kwa mkandarasi wa kampuni ya Sichuan Road and Bridge Group (SABG) anayejenga barabara ya morogoro kufanya kazi usiku na mchana kwa lengo la kuwaondolea changamoto ya foleni wananchi wanaopita njia hiyo.

Maagizo hayo ametoa leo Disemba, 15 2024 jijini Dar es Salaam katika ziara aliyoifanya Gongo la Mboto na Kimara ya kukagua miundombinu ya miradi ya BRT amesema wameanza na mkoa wa Dar es Salaam kwa sababu wageni wengi wanaofika nchini ni lazima waanzie na mkoa huo hivyo kuna umuhimu wa miradi hiyo ifanywe kwa uharaka na ubora unaotakiwa.

Ulega amesema mkandarasi huyo asipoweza kutimiza hayo atamchukulia hatua kali za kisheri.

“Kipande cha mradi wa BRT cha kutoka ubungo hadi kimara bado kinachangamoto hadi sasa mradi huo umefanyika kwa asilimia 26 tu hivyo wapo nje ya muda na wanasababisha msangamano mkubwa wa foleni,”amesema.

Amesema ujenzi wa miundombinu hiyo iendane na uwekaji wa taa za kutosha za barabarani.

“Nataka nione ujenzi wa barabara Nyerere Road ujenzi unaenda kwa haraka kwa sababu barabara ina umuhimu kwa jamii na vizuizi visivyo vya lazima viondolewe ili kupunguza changamoto ya foleni,”amesema

Ulega amewaomba wananchi wa Dar es Salaam kuendelea kuwa wavumilivu kipindi hiki ambacho ujenzi wa barabra katika maeneo mbalimbali nchini

Kwa upande wake Meneja Mradi wa BRT, Mhandisi Frank Mbilinyi amesema ujenzi wa awamu ya tatu ambao upo nyerere road umekamilika kwa asilimia 70 na kwenye mkataba ulitakiwa kukamilika mwezi Machi mwakani.

“Nashukuru na nimefurahi mkandarasi huyu yupo ndani ya muda na ifakapo Machi mwakani anatakiwa kutukabidhi barabara yetu,” amesema.

Naye Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa alimshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuwaletea Watanzania maendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here