Home KITAIFA AFISA UTHIBITI UBORA WA KANDA YA ZIWA ATOA NASAA KWA WANAFUNZI

AFISA UTHIBITI UBORA WA KANDA YA ZIWA ATOA NASAA KWA WANAFUNZI

Mwanza

WANAFUNZI wanaotarajiwa kuanza elimu ya sekondari wameaswa kupokea kwa mtazamo chanya masomo ya amali watakayoanza kusoma mwakani kwani yamelenga kuwaandaa kuwa na maarifa makubwa ya stadi za kazi.

Ushauri huo umetolewa Disemba, 13 2024 na Afisa Udhibiti Ubora wa Elimu Kanda ya Ziwa Lucy Nyanda kwa wanafunzi 54 waliohotimu darasa la saba katika shule Maalumu ya Msingi Claud iliyopo Jijini Mwanza ambao wote wamepata ufaulu wa daraja la kwanza kwenye mitihani yao.

Amesema mitaala hiyo mipya itakuwa ni jawabu kwa wanafunzi wenye kipaji katika fani yoyote kwani atajifunza kwa muda mrefu kwa kusoma na kuwa mahiri hivyo kuweza kufanya vizuri kivitendo.

Nyanda amesema tayari mkoani Mwanza elimu ya amali imeshaanza kufundishwa katika baadhi ya shule za sekondari na kuonesha kuwa na mafanikio ya kuwaandaa wanafunzi kwa kuwa na stadi za maisha.

“Kama mwanafunzi anapenda masomo ya sayansi, ufundi anaanza kujifunza mapema kuanzia anapoanza sekondari hivyo anakuwa mahiri zaidi,” amesema Nyanda.

Mkurugenzi wa shule hiyo Victor Raphael amesema ili kuwaendeleza wanafunzi hao waliohotimu darasa la saba katika shule hiyo mwakani wataanzisha sekondari itakayofundisha kwa umahiri mitaala mipya.

Amesema ushirikiano waliopata kutoka kwa wazazi na walezi wa wanafunzi hao umewezesha wanafunzi waliohotimu darasa la saba katika shule hiyo kupata mafanikio makubwa ya daraja la kwanza.

Naye Padre Felix Magobe amesema kuanzishwa kwa kidato cha kwanza kwa wasichana itawezesha kuandaliwa kwa jamii yenye maadili kwani mwanamke anamchango mkubwa kwenye jamii yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here