Home KITAIFA RAIS DK.MWINYI: TUENDELEE KUTUNZA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025

RAIS DK.MWINYI: TUENDELEE KUTUNZA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025

Zanzibar

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesisitiza jamii kuendelea kuitunza amani iliopo wakati nchi ikielekea katika mwaka wa uchaguzi Mkuu mwakani.

Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo Desemba, 6 2024 alipozungumza na waumini wa dini.ya kiislamu wa Masjid Shaafy uliopo Mombasa Mbuyu Mnene Wiliya ya Magharibi B.

Ameeleza kuwa ni wajibu wa viongozi wa dini na siasa kuwahubiria amani waumini na wafuasi wao ili nchi iendelee kuwa na amani na utulivu ba Serikali iendelee na mipango ya maendeleo.

Aidha Alhaji Dk. Mwinyi amewafahamisha kuwa kwa miaka minne nchi imekuwa na utulivu mkubwa wa kuigiwa mfano hai inayohitaji kuendelezwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Wakati huo huo Alhaji Dk. Mwinyi alifika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Lumumba kuwafariji wagonjwa waliolazwaHospitalini hapo akiwemo Mzee wa chama cha Mapinduzi (CCM), Haji Machano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here