Moja ya basi lililokuwa limebeba wabunge wanaoelekea kwenye mashindano ya michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mombasa nchini Kenya limepata ajali ya kugongana na Lori la mzigo maeneo ya Mbande Kongwa asubuhi ya leo Disemba, 6 2024.
Taarifa iliyotolewa na Bunge imesema majeruhi wa ajali hiyo ambao ni Maafisa wa Bunge wamekimbizwa Hospitali ya Uhuru na Hospitali ya Benjamin Mkapa za mkoani Dodoma.