Dar es Salaam
SERIKALI imesema itaendelea kuhakikisha Wakandarasa na wazabuni wa ndani wanaendelea kujengewa uwezo katika kazi wanazofanya Ili wao wenyewe waweze kupata kipato na kazi zinatolewa na Serikali na waweze kuongeza fursa ya ajira kwa Wananchi ambao wengi wao wanatoka kwenye vyuo mbalimbali hawana ajira.
Hayo yamebainishwa Disemba, 4 2024 jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Elijah Mwandumbya wakati akifungua Mkutano ulioandaliwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Mamlaka za Ununuzi wa Umma(PPRA) kutoka bara na Visiwani.
Amesema lengo la kukutana na Jumuiya
ambao wanataka kufanya kazi katika Miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia Kupokea chagamoto pamoja na Benki hiyo ili kuhakikisha wanapata chagamoto hizo na kutatua Kwa maendeleo ya Tanzania na Wananchi kwa ujumla.
“Zipo chagamoto kadhaa ambazo zingine ni za kimfumo na za kimuundo, kwenye kazi zenu za Kila siku ambazo zina ashiria watanzania wanapaswa kufanya kazi ya ziada Ili kufikia viwango vya kushindina au kutoa huduma inakadiliwa kukidhi viwango vya kuweza kupata kazi wanazo Saini,”amesema.
Amefafanua kuwa katika kuwawezesha wananchi mwaka 2023 Serikali baada ya kupata kibali cha Bunge iliweza kufanya maboresho na kuanzisha Sheria mpya ya ununuzi wa Umma ambayo imetoa fursa kubwa kwa watanzania wanaotoka katika vyuo mbalimbali na hawana ujuzi pia kushiriki kupitia kuzifanya kazi hizo na kuongeza mitaji yao
Amesema Kampuni za hapa nchini zinapata nafasi ya kupata kazi kwa mujibu wa Sheria kwenye kazi zinazotolewa na Serikali Kwa kiwango cha shilingi Billioni 50 kwahiyo ni Sheria ambayo ipo na imewekwa Kwa ajili ya kitafsiri maono ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Amesema sababu imeonekana kwa kiasi kikubwa wazabuni wa ndani watanzania wamekuwa hawapati zabuni za kutosha katika miradi inayofadhiliwa na benki kuu.
Benki ya dunia ilikuwa inapenda kuzungumza nao kupata kutoka kwao changamoto ni nini na wao pia kutoa ufahamu wa nini wanachokifanya,nini kinapaswa kufanyika ili wazabuni waweze kushiriki katika zabuni za benki kuu.
Kwa upande wake Kamishina anayesimamia Maendeleo ya Sera za Ununuzi Umma na Ugavi kutoka Wizara ya fedha, Fredrick mwakibinga amesema mkutano huo uliodaliwa na world Benki kwa kuishirikiana na Mamlaka za Udhibiti wa ununuzi wa Umma kutoka Bara na visiwani.
“Kwa kiasi kikubwa wazabuni wa Tanzania awali walikuwa hawapati zabuni za kutosha zinazofadhiliwa na Benki ya Dunia hivyo wameamua kukutana nao ili waweze kujua ni chagamoto zipo zinazowakabili na mambo gani yalekebishwe,”amesema.
Mwakibinga amesema Lengo ni kuboresha miongozo inayoongoza maeneo hayo ili kutoa fursa za ajira Kwa wazawa na kuhakikisha Kampuni za kitanzania zinapata tenda katika Mashirika mbalimbali ya kimaendeleo.
Ameeleza kuwa ununuzi wa umma umegawanyisha zabuni kwa kutoa upendeleo maalumu jambo ambalo linazuia watu wa nje kutokuja kuwanyang’anya watu wa ndani zabuni hizo.
“Huu ni upendeleo rasmi ambao umefanywa na Serikali ya awamu ya sita imeona izuie baadhi ya maeneo ili watanzania waweze kushiriki peke yao ili waweze kukua na kuimarika zaidi,” amesema.
Mwakibinga ametaja changamoto mbalimbali ikiwemo suala la uelewa kwa kila upande,
kujenga uwezo na kuweka jitihada za kuwaongezea uwezo na bado masuala ya uwezeshaji kimtaji kupata mikopo bado ni chagamoto.