Home KITAIFA RAIS DK.MWINYI ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA ZANZIBAR

RAIS DK.MWINYI ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA ZANZIBAR

Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Zanzibar.

Chuo Kikuu cha Zanzibar kimemtunuku Shahada hiyo ikiwa ni kutambua na kuthamini Mchango wa Uongozi wake Unaoacha Alama na historia itakayokumbukwa wakari wote

Hafla ya kutunukiwa Shahada hiyo imefanyika leo Disemba,5 katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu wakati wa Mahafali ya 22 ya Wahitimu wa mwaka 2024

Shahada hiyo ya Heshima ya Uchumi ametunukiwa kuthamini Mchango wake na Mafanikio makubwa yaliofikiwa Zanzibar hususan Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo yaliopatikana Kipindi kifupi cha Uongozi wake wa miaka minne akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Awali ulisomwa Wasifu wa Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi kabla kutukunukiwa Shahada hiyo uliomuelezea kuwa Kiongozi wa mfano anaewajali watu wake pamoja na Maendeleo ya nchi.

Maeneo mengine ya mafanikio yalioorodheshwa katika wasifu huo ni pamoja Uimarishaji wa Miundombinu ya Barabara na Viwanja vya Ndege hatua inayochochea ongezeko la Watalii na fursa za ajira katika sekta hiyo kwa wananchi

Kuimarika kwa sekta ya Uchumi wa Buluu na matumizi sahihi ya Rasilimali ziliopo nchini.

Uwezeshaji wa Wanachi kiuchumi ikiwemo kuwapatia mikopo ili kuinua kipato chao.

Ongezeko la Bajeti ya Serikali na Pato la Taifa pamoja na kudhibiti kasi ya Mfumuko wa bei.

Eneo jengine ni kuanzishwa kwa miradi ya kimkakati inayosaidia kukuza kwa Uwezo wa Wananchi na Maendeleo ya kiuchumi.

Ongezeko la Pensheni jamii kwa Wazee na uanzishwaji wa Mfumo wa ufuatiliaji wa Ukaguzi wa ndani katika Taasis za Umma .

Ujenzi wa Skuli za ghorofa na kuimarika kwa maslahi ya Walimu ,skuli za ufundi na Elimu Jumuishi.

Kuimarika kwa Sekta ya Afya kwa Ujenzi wa Hospitali za Mikoa na za Wilaya katika Wilaya zote za Zanzibar na Ujenzi wa Viwanja vya Michezo vya New Aman Complex na Gombani Pemba.

Uchimbaji wa Visima vya Maji na Uanzishwaji wa Mfumo wa Sema na Rais uliochangia kwa kiasi kikubwa kutatua matatizo ya Wanachi na kupatiwa Ufumbuzi.

Rais Dk.Mwinyi amekishukuru chuo hicho kwa kuthamini juhudi na kazi anazofanya kwa ajili ya Maendeleo ya nchi.

Ameeleza kuwa Shahada hiyo Itamuongezea kasi na motisha ya kuleta Maendeleo katika nyanja mbalimbali kwa maslahi ya wanachi.

Aidha Rais Dk. Mwinyi amebainisha kuwa Shahada hiyo aliotukuwa Inaakisi kazi nzuri inayoifanya na Serikali anayoiongoza na itamuongezea hamasa ya Maendeleo zaidi.

Rais Dk. Mwinyi amefafanua kuwa ameipokea Shahada hiyo na kuwashukuru Viongozi na Watendaji wote Serikalini kwa kumuunga mkono na Ushirikiano uliopo unaofanikisha kufikiwa kwa malengo ya Maendeleo ya nchi.

Pia ameahidi kuienzi heshima hiyo na kuwahakikishia wananchi kuendelea kuwatumikia wananchi Uwezo wake wote.

Amesisitiza kuwa kutunukiwa kwa Shahada hiyo kuwa sio mwisho wa safari bali mwanzo wa hatua kubwa ya Maendeleo inayokuja katika miaka ijayo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here