Geita
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Geita, Alhaji Adam amewataka vijana kuchangamkia fursa ya kilimo katika kipindi hiki cha mvua Ili kukabili changamoto ya ajira iliyopo nchini.
Akizungumza Leo Disemba, 4 2024 wilayani ya Nyang’hwale amewataka vijana wilayani humo kulima mazao ya Chakula na Biashara Ili waondokane na changamoto za kiuchumi zinazowakabili.
Adam amesema kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu hivyo ni vyema watanzania kutambua umuhimu wa kilimo kuwa itawasaidia kujikomboa kiuchumi na kuondokana na adha zinazowakabili za ukosefu wa ajira katika eneo lao.
Wakati huohuo Mwenyekiti huyo ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha wakulima kupata mbolea na huduma za ughani kuwezesha mapinduzi chanya ya kilimo.